Arusha
Home » » DK SLAA AWALILIA WAKULIMA KARATU, NGORONGORO

DK SLAA AWALILIA WAKULIMA KARATU, NGORONGORO

 MBUNGE Karatu, Dk Wilbrod Slaa, ameitaka Serikali ya Mkoa wa Arusha kuanzisha vyama vya misingi vya ushirika katika Wilaya za Karatu na Ngorongoro, ili viweze kuwasaidia wakulima wa wilaya hizo.

Dk Slaa, alisema hayo juzi kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha kilichofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutao (AICC) kujadili utekelezaji wa mikakati ya maendeleo ya Mkoa wa Arusha.

Alisema wakulima wa wilaya hizo kwa sasa wamekuwa na wakati mgumu wa kupata pembejeo za kilimo mbegu bora pamoja na masoko ya mazao yao kutokana kukosekana kwa vyama imara vya ushirika kwenye wilaya hizo.

Alisema kwa kuwa wakulima hao wanatumia Chama cha Ushirika cha Mkoa wa Manyara (RIVACU), hawanufaiki na chama hicho kwani makao makuu ya chama hicho yapo mkoani Manyara na kwamba wakulima wa Karatu Ngorongoro hawashirikishwi kwenye vikao na mikutano muhimu ya chama.

“Kwa muda mrefu wakulima wetu wamekuwa wanakosa haki yao ya kimsingi japokuwa wamekuwa mstari wa mbele katika uzalishaji wa mazao ya mahindi na vitunguu kwa wingi na kuwa tegemeo katika Mkoa wa Arusha na hata mikoa mingine nchini, hivyo imefika wakati wa serikali kushughulikia jambo hili haraka,” alisema Dk Slaa.

Hoja hiyo pia iliungwa mkono na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Jovika Kasunga ambeye pia alisema kuwa wilaya hizo hazina benki za kutosha na kutoa mfano wilaya yake ina benki mojo ya NMB.
 Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa