Na Woinde Shizza, Arusha
Mamlaka
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta)wametakiwa kuhakikisha
wanasikiliza maoni ya wadau ili kujua mahitaji yao sambamba na kubadili
mitaala ya elimu ya mafunzo yanayotolewa kwenye vyuo hivyo ili kuendana
na soko la ajira lililopo hivi sasa.
Hayo
yanesemwa leo jijini hapa na Waziri wa Kazi na Ajira Mhe Gaudensia
Kabaka wakati alipokuwa akizindua kongamano lililoshirikisha wadau
kutoka sekta mbalimbali kwaajili ya kujadili changamoto wanazozipata
wadau hao na nini chakuongeza kwa vijana wanaopitia Veta na kupata ajira
katika sekta mbalimbali sanjari na kuzindua kitabu kinachoanisha
mahitaji ya soko la ajira kwa vijana
Mhe
Kabaka aliwataka vijana kutumia fursa za kujiunga na Veta ili waweze
kujiariri badala ya kufanya biashara za kuuza vitu mikononi bali
watumie taaluma walizozipata kuzalisha vitu vyenye ubora.
Alisema vijana wanaopitia vyuo vya mafunzo Veta si wengi sana huku wimbi
la vijana likiwa bado mitaani na kuuza bidhaa zao mabarabarani hivyo ni
vyema sasa vijana hao wakaondoka barabarani na kujiunga na vyuo vya
ufundi ili waweze kupata mbinu za kutengeneza vitu sambamba na kupata
masoko ya uhakika.
Alisema
ni vyema sasa Vyuo vya Veta vikaweka mkazo katika sekta ya madini na
gesi ili waweze kuangalia mahitaji ya wataalam ni yapi na kutoa elimu
hiyo ambayo itawezesha vijana wengi kupata ajira na kukuza uchumi
wananchi.
"Mahitaji
ya vijana ni mengi katika sekta rasmi na zisizo rasmi na kia sekta
inamtegemea mtu fulani hivyo ni vyema Veta mkasikiliza mahitaji ya wadau
sambamba na kutafuta mbinu za kufundisha zaidi ili kuendana na mahitaji
ya soko na nyinyi vijana tokeni barabarani mkajiunge na vyuo vya ufundi
ili kuweza kuuza biashara zenu kwa ubora badala ya kukimbilia kuuza
barabarani ". Alisema Mhe Kabaka
Naye
Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi alisema kongamano hilo
hufanyika kila mwaka na kushirikisha wadau katika sekta mbalimbali ili
kujadili masuala mbalimbali na mahitaji ya wadau hao katika sekta ya
ajira sambamba na kuboresha mitaala itakayokwenda na wakati na kuwezesha
vijana wanaopitia Veta kuwa bora zaidi kipindi cha kumaliza chuo na
kupata ajira.
Alisema
pia Veta inakabiliwa na uhaba wa rasilimali fedha kwenye ujenzi wa
vyuo vipya kwenye Wilaya mpya ambazo ni Katavi, Geita, Njombe na Simiu
lakini pia kuonaongezeko kubwa la vijana na watu mbalimbali ambao
wanajiunga na vyuo hivyo nchini kwaajili ya kupata mafunzo mbalimbali
yanayowawezesha kupata ajira.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya Veta, Profesa Idrissa Mshoro alisisitiza kuwa
Veta inatambua na kuthamini maeneo mbalimbali yanayohitaji soko la ajira
ndio maana vijana wanaopata ujuzi kupitia veta wanafanya kazi kwa
makini na kujipatia vipato zaidi.
Aliongeza
kuwa hivi sasa Veta inashirikiana na tasisi na mashirika mbalimbali
hususan ya sekta ya madini na gesi na kutoa mafunzo kwaajili ya
kuwasaidia vijana kukabiliana na soko la ajira .
WAZIRI wa
Kazi na Ajira Mhe. Gaudensia Kabaka wakati alipokuwa akizindua kongamano lililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwa ajili ya
kujadili changamoto
wanazozipata wadau hao
Wadau wakifuatilia mada
waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha wakimuoji mwenyekiti wa bodi |
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment