Arusha
Home » » KAMPUNI ZASHINDANIA RUZUKU YA REA

KAMPUNI ZASHINDANIA RUZUKU YA REA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

KAMPUNI binafsi 55 za kuzalisha umeme nje ya Gredi ya Taifa zinashindana kupata nafasi 20 ya ruzuku kwa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kuweza kuzalisha umeme na kusambaza kwa taasisi na watu binafsi katikavijiji mbalimbali hapa nchini.
Taasisi hizo ambazo zimeandika andiko la mradi na kuwakilisha kwa wakala huo jana zilikuwa zinaelezea na kuonyesha baadhi ya vifaa inavyotumia kufanikisha mradi husika kama vitapata fursa hiyo kwa muda utakaokubalika.
Akizungumza na Tanzania Daima baada ya kutembelea maonyesho ya taasisi hizo zinazoshindana, Mkurugenzi idara ya nishati na Petroli wa Wizara ya Nishati na Madini, Injinia Hosea Mbise alisema, ushindanishwaji huo ni moja ya kanuni kuwezesha kampuni iliyokidhi viwango kupata nafasi hiyo.
Alisema kampuni zote zikiwemo za wazalendo zimeonyesha ubora wa kazi zao lakini zinazohitajika kufanikisha miradi husika kwa mwakahuu wa fedha ni 20 pekee kati ya 55 zinazoshindana .
“Wakala umetenga fedha kiasi cha shilingi bilioni 4.6 kwa ajili ya utekelezaji wa umeme vijijini ambao kwa kiasi kikubwa utahusisha umeme wa jua na upepo ambao gharama zake ni nafuu kwa wananchi wa kipato cha chini hivyo kuhitaji kampuni bora zenye uwezo wa kuzalisha umeme huo bila matatizo,’’ alisema.
Mmoja wa washindani katika kinyang’anyiro hicho ni Ansi Mmasi mkurugenzi wa kampuni ya Baraka Solar Specialist ambaye anaomba kupata nafasi ya kutoa huduma ya uzalishaji umeme katika Wilaya ya Bagamoyo kwa mradi utakaojulikana kama ‘Kibindu Village Solar Mini grid’ ambapo jumla ya wakazi 440 wataunganishiwa umeme huo.
Mmasi alisema kutokana na ukomavu wa kampuni yake na kukua kwa teknolojia ya uzalishaji umeme wa njia ya jua wanatoa huduma ya kusambaza umeme huo kwa njia kama za Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) kwa kutumia nyaya na pia kulipia bili kwa njia za mita za umeme.
Wakala wa Umeme Vijijini imejiwekea malengo ya kuhakikisha vijiji vyote 15 000 hapa nchini vinapata umeme wa uhakika ifikapo mwaka 2025 ili kusaidia kupunguza makali ya maisha na kuongeza uzalishaji na vipato kwa wakazi wa maeneo ya vijijini.

Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa