Home » » SAMUNGE KUFURAHIA UMEME NAFUU

SAMUNGE KUFURAHIA UMEME NAFUU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Neema ya huduma za umeme imewaangukia wakazi wa Kijiji cha Samunge, Wilaya ya Ngorongoro, Mkoa wa Arusha baada ya Kampuni L’s Solutions kushinda ufadhili wa Dola za Marekani 100,000 kusambaza nishati hiyo katika eneo hilo.
Wakazi hao walioanza kuona nuru ya huduma za kijamii baada ya kugunduliwa dawa ya ‘kikombe cha babu’ iliyokuwa ikitolewa na Mchungaji Ambilikile Mwasapile mwaka 2011, sasa wanatarajia kusambaziwa umeme wa bei nafuu.
Ufadhili huo umetolewa na kupitia Kampeni ya ‘Power Africa’ iliyoanzishwa na Rais wa Marekani, Barrack Obama, huku kampuni 300 zikishindanishwa.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo Anord Nzali alisema jana kuwa umeme huo utauzwa kwa bei nafuu kuanzia Sh800.
Kampuni nyingine zilizoshinda ni Jamii Power, Lung’ali Natural Resources na Space Engineering.
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa