Home » » IIED: WATETEZI HAKI ZA BINADAMU WASAIDIWE

IIED: WATETEZI HAKI ZA BINADAMU WASAIDIWE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

JAMII imeshauriwa kutoa msaada kwa watetezi wa haki za binadamu katika maeneo yao ili kujenga misingi bora.
Ushauri huo umetolewa jana jijini hapa na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo na Mazingira (IIED), Alais Morindat, katika mafunzo ya siku tatu ya watetezi wa haki za binadamu kwa jamii za wafugaji.
Morindet, alisema dunia inapita katika wakati mgumu wa mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kiteknolojia, hivyo ni vyema suala la utetezi wa haki za baadhi ya makundi madogo madogo lizingatiwe.
“Uwepo wa makundi ya watetezi kupitia mitandao na taasisi mbalimbali ni muhimu katika jamii na hivyo yanapaswa kuhakikisha inayalinda dhidi ya madhara yoyote ili yaweze kutimiza wajibu wao bila woga,” alisema.
Nae Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka mtandao wa watetezi wa haki za binadamu, Onesmo Olengurumwa, alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kutambua haki zao watetezi wa haki za binadamu.
Aidha, alisema mtandao huo umeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia watetezi wa haki za binadamu wanapokumbwa na matatizo mbalimbali wakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa