Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MTU mmoja anayedaiwa kuwa jambazi sugu maarufu kama Ramadhani Jumanne ‘Rama Ndonga’ (37) ameuawa katika majibizano ya risasi kati yake na polisi yaliyotokea usiku wa kuamkia jana katika kijiji cha Moivo, Arumeru mkoani Arusha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Liberatus Sabas alisema, kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa anatafutwa kwa muda mrefu kutokana na kuhusika katika matukio mbalimbali yakiwemo ya mauaji ya Sakina.
Kamanda alisema kuwa polisi walitumia mbinu za kipelelezi na kufika nyumbani kwa mtuhumiwa usiku wa manane na kumwamuru marehemu (mtuhumiwa) kujisalimisha lakini alikaidi na kuanza kuwarushia risasi hatua iliyopelekea kujibu mapigo na kusababisha kifo chake.
Alisema kuwa marehemu alihusika katika matukio mbalimbali likiwemo lililotokea Agosti 21, mwaka huu ambapo akiwa eneo la Olasiti alimjeruhi kwa risasi mtoto mdogo Christen Nickson (3) kwa kumpiga risasi mdomoni iliyotokea kichwani na kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru.
Alisema kuwa polisi walifanya upekuzi nyumbani kwa marehemu na kufanikiwa kukuta bastola aina ya Glock 19 yenye namba RLU976 iliyotengenezwa nchi Australia ikiwa magazine yenye risasi 14.
Kamanda alisema pia marehemu alipatikana na magazine moja yenye risasi 15 na magazine mbili zenye uwezo wa kubeba risasi 30 kila moja, redio ya upepo yenye namba ITSS/UNICTR inayodaiwa kuporwa kwenye mahakama ya kimbari ya Rwanda.
“Alikutwa na pikipiki aina ya Toyo Power King yenye namba T.507 BSU, kofia ngumu ya kuendeshea pikipiki, pingu pamoja na vifaa vya kusafishia bastola na koti jeusi,” alisema
0 comments:
Post a Comment