Arusha
Home » » CHAVITA WALIA NA UKOSEFU WA WATAALAM

CHAVITA WALIA NA UKOSEFU WA WATAALAM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

CHAMA cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kimeiomba serikali kuwasaidia katika kutatua matatizo yanayowakabili ya ukosefu wa wataalamu wa lugha za alama inayowakabili kundi hilo.
Hayo yalisemwa jana na Mwakilishi wa chama hicho mkoa wa Arusha, Malise Swila wakati akizungumzia changamoto mbalimbali zinazokikabili chama hicho .
Alisema kuwa matumizi ya lugha za alama na wataalamu wa kutosha utawawezesha kupata fursa nyingi za kushiriki katika masuala mbalimbali ya maendeleo katika Taifa ambayo kwa sasa wanayakosa kutokana na lugha hiyo kutotambulika rasmi.
Alisema kuwa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali za kijamii kama vile afya, elimu, ajira na ushirikishwaji hafifu katika masuala mbalimbali ya kijamii.
Swila alisema kuwa kutokana na kukosekana kwa walimu wenye kujua kutumia lugha hiyo, kundi hilo limekuwa likikosa elimu bora.
Naye Mkuu wa wilaya ya Arumeru , Nyirembe Munasa alisema , serikali itaendelea kuweka mikakati mbalimbali katika kuhakikisha kuwa viziwi wanapata haki zao za msingi .
Munasa alikitaka chama hicho kuhakikisha wanakuwa na miradi endelevu ambayo itawasaidia kujileta maendeleo sambamba na kutatua changamoto zilizopo miongoni mwao.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa