Meneja Mkuu wa Samsung Mr Mike Seo akiwahutubia wanahabari(hawapo kwenye picha) katika uzinduzi rasmi wa duka la kielektroniki la Samsung na kituo cha huduma kwa wateja mjini Arusha. |
Meneja wa Usambazaji wa Samsung akitoa maelezo kwa wateja na waandishi wa habari. |
Meneja Mkuu wa Samsung Mr Mike Seo akiwahutubia wateja wa Samsung katika uzinduzi rasmi wa duka la kielektroniki la Samsung na kituo cha huduma kwa wateja mjini Arusha. |
Meneja wa huduma Samsung Mr Mubarak Mikidad akiwahutubia wanahabari katika uzinduzi rasmi wa duka la kielektroniki la Samsung na kituo cha huduma kwa wateja mjini Arusha. |
Na Gadiola Emanuel -Arusha
Kampuni ya Samsung inazindua rasmi siku ya leo
duka kubwa na kituo chake cha huduma kwa wateja lililopo barabara ya Sokoine
mjini Arusha. Uzinduzi huo utawawezesha wateja wake wote mkoani Arusha kupata
huduma stahiki na bidhaa halisi za Samsung. Kituo hiki ni cha kwanza
kuzinduliwa mkoani Arusha na kampuni hii kubwa yenye idadi kubwa ya watumiaji
na vifaa bora vya kielektroniki ulimwenguni.
“Mtazamo wa maisha ya wateja hubadilika
kwa kasi kubwa na kuwafanya kuongeza mahitaji ya bidhaa na huduma bora. Kama
kampuni kubwa inayoongoza kuwa na vifaa bora vya kielektroniki ulimwenguni,
Samsung imefanya juhudi kubwa kuhakikisha inatimiza mahitaji ya wateja wake
wote Afika. Mkoa wa Arusha hutegemea sana biashara kwani una wakaazi toka jamii
mchanganyiko. Hivyo katika Afrika Mashariki, Arusha ni kitovu cha wageni toka
nchi mbalimbali ulimwenguni. Kampuni ya Samsung ina imani kubwa kwamba kituo
cha huduma kwa wateja kitatoa ushirikiano mzuri na kuboresha uhusiano kwa wateja
wake mkoani Arusha. Kwasababu Arusha ni muhimu na kituo kikuu cha safari nchini
Tanzania”, haya yamesemwa na
Mkurugenzi mkuu wa kampuni hii nchini Tanzania, Bw. Seo
Mbali
na kuuza simu za mkononi na bidhaa za kielektroniki, duka hili jipya la Samsung
litatoa huduma za ziada kwa wateja wake. Hii ni pamoja na kuwapa wateja wake
watakaojisajili na uduma ya e-warranty
usaidizi wa kiufundi bila malipo kwa kipindi cha miaka miwili.
Mpango
huu utawanufaisha wateja wa Samsung kwa kusajili bidhaa zao kupitia Simu. Huu
ni mchakato utakaofanyika kwa kutuma namba IMEI kwenda 15685. Baada ya kufanya
hivyo wateja watanufaika na msaada wa kifundi kwa kipindi cha miaka miwili
sambamba na kujipatia nafasi ya kushinda bidhaa mbalimbali za Samsung.
Katika
kusherehekea uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja ambacho kinawasogezea
wateja wake huduma karibu, kampuni hii kubwa duniani inawaletea habari njema
wakaazi wa Arusha kwa kutoa punguzo kubwa la bei za bidhaa zake. Kwenye kipindi
hiki cha ufunguzi bidhaa zitakazokuwa na punguzo la bei ni pamoja na; Luninga, feni,
majokofu na vifaa vya nyumbani. Bila kuwasahau wateja wake wa simu, ambao
watapewa wa bure vifurushi vya intaneti na zawadi za T-shirts zitatolewa
kwaajili ya wanunuzi wa simu na vifaa aina ya Galaxy.
Kwa sasa nchini Tanzania
kampuni ya Samsung ina maduka na vituo vya huduma kwa wateja katika mikoa ya
Mwanza na Dar es Salaam na ina mipango kabambe kuongeza huduma zake mikoa
mingine.
Duka hili na kituo chake
cha huduma kwa wateja vitatoa huduma siku za wiki yaani Jumatatu-Ijumaa kuanzia
saa 9.30 asubuhi hadi 5.00jioni kwa Jumamosi ni kuanzia saa 9.30asubuhi hadi
1.00 mchana, litafungwa siku za Jumapili na Siku kuu.
Kuhusu Vifaa vya kielektroniki
vya Samsung
Teknolojia ya Samsung inatumiwa
na watu takribani 236,000 katika nchi 79, inaleta mabadiliko na kuiwezesha
dunia kuingia kwenye teknolojia mpya na
matumizi ya smart phone, luninga, air-conditioner, vifaa vya nyumbani vya
kieletroniki, kamera, na vifaa vya maofisini kama kompyuta na printers ambavyo
vina teknolojia ya hali ya juu kukidhi mahitaji ya wateja. Kujifunza mengi zaidi,
tembelea www.samsung.com na www.facebook.com/Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment