Home » » ARUSHA KUANDAMANA LEO

ARUSHA KUANDAMANA LEO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo, (CHADEMA), mkoani hapa, Amani GolugwaMWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo, (CHADEMA), mkoani hapa, Amani Golugwa, amesema kuwa watafanya maandamano ya amani leo wakiwa wamefunga vitambaa vyeupe mkononi.
Aidha, amelitaka Jeshi la Polisi kufahamu kuwa, utii wa sheria bila shuruti unategemea uwezo wa jeshi hilo kusimamia sheria bila ubaguzi, huku wakishangazwa na hatua ya polisi kuzuia mikutano bila kuwapa maelezo ya kina juu ya sababu iliyowafanya kufikia uamuzi huo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya
maandalizi ya maandamano hayo yanayotarajia leo kuanzia maeneo ya Philips majira ya saa 5 asubuhi, alisema wameamua kuendelea na mandandalizi ya maandamano na mkutano baada ya kushauriana na mawakili wa chama hicho.
Alisema wamejiridhisha kuwa kuna mapungufu mengi ya kisheria kwenye majibu ya polisi, kupitia barua yao ya kuwakataza wasifanye mikutano yenye Kumb. Na. AR/B.5/VOL.IV/5 ya Septemba 18, mwaka huu.
“Barua hiyo haijatueleza ni lini na ni Mamlaka gani imepiga marufuku maandamano ya chama chochote cha kisiasa na kwa sababu gani, kwani tujuavyo sisi, nchi yetu haimo vitani wala hatujasikia taarifa
ya tukio lolote linalohatarisha amani ya jumla nchini mwetu, wala katika wilaya yetu ya Arusha,” alisema Golugwa.
“Tunasikititishwa na zuio maandamano na mkutano wetu lililotolewa na polisi, kwani ni la kibaguzi na lenye lengo la kutunyima fursa ya kutoa maoni yetu ya kisiasa, juu ya ufisadi wa kodi za Watanzania unaofanywa na Bunge Maalum la Katiba huku likishindwa kutupa tarehe nyingine tunayoruhusiwa kufanya mikutano…
“ Tunalikumbusha jeshi la polisi kuwa chini ya sheria ya vyama vya siasa (The Political Parties Act, Cap 258) kifungu cha II, CHADEMA ina haki ya kupewa ulinzi na usaidizi wa vyombo vya usalama (security
agencies) kwa ajili ya kuendesha mikutano yake kwa amani na utulivu,”  alisema Golugwa.
Alisema kuwa, sababu nyingine iliyowafanya waendelee na maandamano ni kuwa, polisi hawajawafafanulia ni vipi maandamo na mkutano wao utasababisha uvunjifu wa amani.
“Polisi wanajua CHADEMA tuna uwezo wa kusimamia mikusanyiko ya wanachama na wafuasi wetu kwa umakini wa hali ya juu. Sisi ni vinara wa dhana ya polisi jamii kwenye mikusanyiko ya chama chetu. Ninyi waandishi ni mashahidi tumewahi kuandamana wenyewe bila ulinzi wa polisi na hakuna mtu aliyeumizwa wala kuibiwa,” alisema Golugwa.
Mikutano ya CHADEMA inatarajiwa kufanyika leo kwenye majimbo yote saba ya mkoa huu yakiongozwa na wabunge wa chama hicho.
Hata hivyo, Kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas, ameweka wazi msimamo wa jeshi hilo kuwa maandamano hayo hayaruhusiwi.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa