Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Meneja Biashara wa Kampuni ya Kuhudumia Makontena Bandarini, Predi
Assenga (kushoto) na Meneja wa Kitengo cha Makontena, Donald Talawa
wakiangalia meli ya kubeba mitambo mizito Zhen Hua wakati ikitia nanga
Dar es Salaam jana
Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Dk Richard Sezibera
amesema nchi wanachama wa jumuiya hiyo zinajengwa na sekta binafsi
ambayo ndiyo injini ya uchumi wake.
Akizungumza baada ya kufungua duka la Nakumatt
jijini Arusha, Dk Sezibera alisema: “Tunaamini kuwa sekta binafsi ndiyo
injini ya uchumi wa Afrika Mashariki na sisi tutahakikisha wananchi wa
nchi wanachama wanafaidika na ukuaji wa uchumi wa jumuiya kupitia fursa
za kibiashara zinazopatikana EAC.”
Kampuni ya Nakumatt iliyonunua mali zote
zilizokuwa chini ya maduka ya Shoprite nchini, imewekeza zaidi ya Dola
za Marekani 2 milioni (Sh3.3 bilioni) mkoani Arusha na kuwawezesha
vijana 50 kupata ajira za kudumu.
Dk Sezibera aliupongeza uongozi wa kampuni hiyo
kwa kufungua duka hilo. Ufunguzi huo unafikisha idadi ya maduka ya
Nakumatt (Nakumatt Supermarkets) katika nchi zote za EAC kufikia 50,
huku Tanzania ikiwa na manne.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Nakumatt, Atul Shah
alisema kuwa ndoto yake ya muda mrefu ni kuwekeza sehemu kubwa ya Afrika
na kuwafaidisha maelfu ya wakulima na wenye viwanda.
Alisema sera ya kampuni yake ni kuendeleza wakulima na wazalishaji wa nchi za Afrika, ambako kampuni hiyo inafanya nao biashara.
Meya wa Jiji la Arusha, Mstahiki Gaudence Lyimo
alisema kuwa kufunguliwa kwa duka hilo kutaongeza hadhi ya jiji hilo na
kuomba wawekezaji wengine kujitokeza kuwekeza.
“Tumefurahishwa na uwekezaji huu…biashara hii
italeta huduma zenye unafuu kwa watu wa kada za juu, kati na chini na
utatuongezea mapato,” alisema Lyimo.
Nakumatt ambayo tayari ina maduka Mlimani City na
Kamata jijini Dar es Salaam na Moshi mkoani Kilimanjaro na Arusha,
imeajiri jumla ya watu 7,500 katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na
Rwanda.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment