Dada wa Lucas Lomayany Molel (37) anayesakwa kwa kumuua
mkewe wa ndoa, Agnes Lucas (24), akiwa katika chumba kilichotumika kwa mauaji
hayo.
Chanzo cha habari kimeliambia Amani kuwa, tukio hilo la
kutisha lilitokea usiku wa kuamkia Julai 7, mwaka huu, nyumbani kwa mtuhumiwa
ambapo baada ya kutekeleza mauaji hayo aliufunika mwili wa marehemu kwa shuka
na kuendelea kulala nao kitandani hadi alfajiri alipotoroka.
Akisimulia kuhusu mauaji hayo, ndugu wa marehemu aitwaye
William Lomayany alisema usiku wa tukio, saa 4, mtuhumiwa alirejea nyumbani
kwake na kutomkuta mkewe, akamsubiri hadi saa 6 usiku, mke akarejea.
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linamsaka kwa udi na uvumba,
muuza nyama jijini hapa, Lucas Lomayany Molel (37) mkazi wa Ilboru kwa madai ya
kumuua mkewe wa ndoa, Agnes Lucas (24) kwa kumcharanga na sime kwa kile
kinachoelezwa kuwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.
Godoro la kitanda alipokuwa analala marehemu, Agnes likiwa
limechafuka kwa damu.
Alisema marehemu baada ya kufunguliwa mlango na kuingia,
alivua nguo zote na kubaki na ‘kufuli’ ambapo alijifunga kanga na kupanda
kitandani kulala. Mtuhumiwa alimfuata chumbani na kumhoji kuhusu kuchelewa
nyumbani hadi muda huo na ndipo mzozo ulipoanza.
William alizidi kusema kuwa, wawili hao walianza kugombana
kwa maneno lakini baada ya muda hali ya utulivu ilirejea, ndipo asubuhi
ilipopatikana taarifa za kuuawa kwa Agnes jambo lililotafsiriwa kuwa huenda
utulivu huo tayari Agnes alishauawa.
Ndoo ikiwa na damu ya Marehemu Agnes Lucas.
Inadaiwa kuwa, mtoto wa kwanza wa mtuhumiwa, Jessica Lucas
(11) ndiye aliyekuwa wa kwanza kufungua mlango wa chumbani kwa wazazi wake na kumkuta mama yake
amelala na damu chapachapa, akaenda kutoa taarifa kwa majirani.
Ilidaiwa kuwa, baada ya taarifa hiyo, majirani waliingia
ndani ya chumba hicho na kuukuta mwili wa marehemu ukiwa umelala kwenye dimbwi
la damu huku akiwa mtupu.
Agnes Lucas, enzi za uhai wake, akiwa kwenye picha ya pamoja
na mumewe, Bw. Lucas Lomayany Molel.
Akizungumza mbele ya askari polisi waliofika kushuhudia
tukio hilo, Jessica alisema baba yake alimwamsha usiku akimtaka atoke kufunga
mlango baada ya kutoka ndani. Akajua baba yake anakwenda kazini kama ada.
“Nilikwenda kufunga mlango, baba aliondoka bila kusema
chochote. Lakini jana usiku (Julai 6) baba alimpiga sana mama na alinipiga na
mimi wakati namwambia amsamehe,” alisema Jessica.
Majirani wa wanandoa hao, wamelaani mauaji hayo na kusema
Lucas hakupaswa kumuua mkewe badala yake angewashirikisha watu wengine wakiwemo
wazazi wamkanye kama alikuwa akimsaliti.
“Kwa jinsi Lucas alivyokuwa mpole sikutegemea kama angemuua
mkewe kikatili, kama alikuwa akimsaliti
angewaeleza wazazi wake ili wamkanye,” alisema jirani yao ambaye hakupenda jina
lake liandikwe gazetini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alikiri
kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa, uchunguzi unaendelea na jeshi lake linamsaka mtuhumiwa
huyo.CHANZO GPL
0 comments:
Post a Comment