Home » » MTEI; NILILIPWA MSHAHARA SAWA NA MWALIMU NYERERE

MTEI; NILILIPWA MSHAHARA SAWA NA MWALIMU NYERERE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Inawezekana likawa jambo nadra kutokea kwa sasa, lakini enzi za uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere lilitokea.
Ni baada ya mwasisi huyo wa Taifa kuamua kwa hiari kupunguza mshahara wake kwa asilimia 10 ili kupunguza pengo baina ya maskini na wale wenye kipato cha juu, uamuzi ambao ulifuatwa na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakati huo, Edwin Mtei.
Mwaka 1968, Mwalimu Nyerere aliyekuwa akilipwa mshahara wa Sh5,000 kwa mwezi alikiona ni kiasi kikubwa ikilinganishwa na wengi wa watumishi na hivyo kuamua kukipunguza.
Mshahara huo wa Mwalimu Nyerere ni sawa na ambao alikuwa akilipwa pia Gavana Mtei. Kutokana na punguzo hilo, mishahara yao ilishuka hadi Sh4,500 kwa mwezi.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake Tengeru, nje kidogo ya Mji wa Arusha Jumatatu iliyopita, Mtei alisema alifikia uamuzi huo wa kupunguza mshahara wake baada ya Mwalimu Nyerere kutangaza kupunguza mshahara wake.
Alisema: “Nilipunguza mshahara wangu tena kwa hiari yangu baada ya kuona Mwalimu Nyerere amepunguza wa kwake.”
Alisema wakati ule mshahara wa Gavana ulikuwa ukipangwa na Serikali na kwamba ulikuwa na kipengele katika mkataba kikionyesha kuwa hauwezi kupunguzwa na mamlaka yoyote, labda atakapotaka mwenyewe.
Mtei ambaye pia ni mwasisi wa Chadema alisema sababu nyingine iliyomsukuma kupunguza mshahara wake ni kuona kwamba kama asingefanya hivyo, basi angemzidi mshahara Rais (Nyerere), kitu ambacho kwake hakukipenda.
Alisema, ingawa Mwalimu Nyerere alipunguza mshahara, lakini yeye kisheria hakuwa akibanwa kufanya hivyo kutokana na mkataba wake ambao ulikuwa ukiibana Serikali kutokuugusa mshahara wake.
Alieleza kuwa ukimwondoa yeye na Mwalimu Nyerere, Serikali iliamua kuwapunguzia mishahara watumishi wengine wa kada nyingine serikalini ili kubana matumizi.
“Watu wote walipunguziwa mishahara kuanzia vigogo wote (wa wakati ule),” alisema Mtei ambaye Jumamosi iliyopita alitimiza miaka 82 tangu kuzaliwa kwake.
Sababu za punguzo hilo
Alisema Serikali ya Mwalimu Nyerere iliamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona kuwa kulikuwa na pengo kubwa la kipato kati ya watumishi wa ngazi za chini na wale wa juu.
Mwanasiasa huyo ambaye aliteuliwa kuwa Gavana wa BoT akiwa na umri wa miaka 32, jambo ambalo ni mara chache kufanyika kwa vijana kuaminiwa na hata kupewa madaraka makubwa kiasi kile, alisema Mwalimu Nyerere alimwamini kwa kiasi kikubwa.
Kuhusu Mwalimu Nyerere, Mtei alisema alikuwa kiongozi mwadilifu, ndiyo maana akafanya uamuzi mgumu kama huo wa kugusa mshahara wake mwenyewe.
Alisema kwa kizazi cha sasa ni watumishi wachache wa kuweza kuwalinganisha naye.
Alisema baada ya Mwalimu Nyerere kuondoka katika uongozi wa nchi, watumishi na hata viongozi walibadilika na kujiingiza katika mambo mengi yakiwamo yale ambayo yanakwenda kinyume na maadili.
Uongozi wa sasa
Mtei ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha kabla ya kuteuliwa kuwa Gavana wa BoT alisema katika mazingira ya sasa hakuna kiongozi yeyote ambaye anaweza kukubali au kupunguza mshahara wake.
“Katika mazingira ya sasa, jambo hilo haliwezekani kabisa,” alisema. Aliongeza: “Hivi sasa viongozi wengi wanashindana kupeleka na kuficha fedha Uswisi, wengi wao wanakimbilia kwenye utajiri, si utumishi.”
Alisema hivi sasa viongozi wengi wametanguliza mbele masilahi yao na wengine kujiingiza kwenye ufisadi na hivyo kushindwa kuwatumikia wananchi ipasavyo.
Mtei alisema viongozi wote lazima waongozwe na uzalendo na kuwahurumia wananchi wengi ambao ni maskini.
Alisema uamuzi walioufanya yeye na Mwalimu Nyerere hivi sasa unaweza kufanyika katika chama kingine kinachojali wananchi endapo kitaingia madarakani, ambacho hata hivyo alisema siyo CCM

Chanzo;Mwananchi

0 comments:

Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa