Mzee
wa kanisa la Waadventista wasabato mtaa wa kijenge Agrey Tumaini
akigawa mahindi kwa wananchi wa kitongoji cha kitongoji cha
Nyamagana kilichopo katika kijiji cha Themi ya simba wilayani Arumeru
MKoani Arusha (picha na woinde shizza,Arusha
========= ====== ======
Na Woinde shizza,Arusha
Zaidi
ya wananchi 50 wa kitongoji cha Nyamagana kilichopo katika kijiji
cha Themi ya simba wilayani Arumeru MKoani Arusha ambao waliathiriwa na
mafuriko yaliotokea mwisho mwa mwezi wa nne mwaka huu wamepatiwa msaada
wa chakula na nguo kijijini hapa.
Akikabidhi
chakula hicho mzee wa kanisa la Waadventista wasabato mtaa wa
kijenge Agrey Tumaini alisema kuwa wameamua kuwasaidia wananchi hawa
kutokana na janga ambalo liliwakuta la kuingiliwa na mafuriko ya
maji ambapo yaliwasababishia nyumba pamoja na mazao yao kuezuliwa na
maji hayo
Alisema
kuwa wao kama kikundi cha WAMO kutoka katika kanisa hilo waliguswa
sana na tatizo hili ambalo liliwatokea hivyo wakaamua kujichanga na
kununua vyakula ivyo na nguo kwa ajili ya wahanga hao wa mafuriko.
Alisema
kuwa wameweza kutoa gunia kumi za mahindi ,maharage kunia tatu,unga wa
ugali pamoja na nguo kwa ajili ya watoto wa wananchi ambao walikubwa na
janga hilila mafuriko.
“sisi
tumeguswa sana na tukio hili wenzetu kukubwa na mafuriko kwa kweli
wameadhirika vikubwa kwani wengine awana sehemu zakukaa wengine walikuwa
wamelima mazao yao kama mahindi yaliezuliwa na mafuriko hayo yaani
kiukweli hadi sasa kuna watu awajui wataishije kwa mwaka huu lakini
tumeona sio vibaya iwapo tukiwasaidia ichi kidogo tulichonacho maana
ata neno la mungu linasema katika mathayo uwa mlikuja na njaa nikawapa
chakula,mlikuja uchi nikawavisha sasa na sisi tumeamua kuwapa ichi
kidogona tunawaomba watu wengine waendelee kujitokeza kwa wingi
kuwasaidia wananchi hawa kwani wapo katika mazingira magumu sana”alisema
Tumaini.
Akipokwa
msaada huo mmoja wa wananchi hao alietambulika kwa jina la Gidion
Maganga alisema kuwa anashukuru sana kanisa hili la wa sabato kwa kuja
kuwasaidia kwani kuna baadhi yao walikuwa hawajui hatima ya maisha yao
kwani ata chakula kwao kupata ni tabu .
Alisema
kuwa pamoja kuwa kuna baadhi yaviongozi na taasisi ambazo zimewapelekea
chakula kama maindi ,magodoro pamoja na nguo lakini bado wanaitaji
maada kwani mvua zile ziliwachukulia vitu vyao vingi ikiwemo mazao
maindi waliokuwa wameyaifadhi ndani vyombo ,magodoro na sio ivyo tu
lakini pia zileweza kumuua mwananchi mmoja.
Akizungumzia
tukio hilo mwananchi mungine ambaye aliyejitaja kwa jina la Zainabu
Minja alisema kuwa siku hiyo ya tukio lilitokea majira ya saa saba usiku
wakati wamelala huku mvua ikinyesha ndipo gafla waliona maji mengi
yamekuja na kujaa ndani ya nyumba kitu ambacho kiliwaogopesha zaidi ni
pa le maji yale yalivyoanza kusomba vitu.
“yaani
ndugu muandishi usione apa yaani maji yalikuja na kasi unaona hii chuma
ina uzitowa kilomia ndio niliichukuwa nikaishika na uyu ni mama yangu
na unamuona alivyo mzee nilimwambia ashikilie iyo chuma akashika
mwishowe mikono ikafa ganzi ndipo nikachukua kanga na kumfunga kiunoni
nikaunganisha na chuma ili asipelekwe na maji ila nashukuru mungu
alituona pamoja vitu vilizolewa lakini sisi ni wazima kwakweli”alisema
bi Zainabu
Alitoa
wito kwa wananchi serekali pamoja na taasisi mbalimbali kujitokeza kwa
wingi kuwasiaidia kwani wapo katika halingumu sana katika kipindi
hichi.
0 comments:
Post a Comment