Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Monduli. Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa amezindua mradi wa
maji wa Bwawa la Leken katika Kijiji cha Selela uliogharimu Sh1.1
bilioni, huku akiupongeza uongozi wa Rais Jayaka Kikwete kwa kusaidia
kuondoa tatizo hilo kwa binadamu na mifugo wilayani hapa.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo
juzi, Lowassa, ambaye ni mbunge wa jimbo hilo tangu mwaka 1995, alisema
chini ya uongozi wa Rais Kikwete, Monduli imepata manufaa makubwa na
akawataka wakazi wa jimbo hilo kumpongeza.
Lowassa alisema alipochaguliwa kwa mara ya kwanza
kuwa mbunge jimboni hapa, changamoto aliyoikuta ilikuwa ni ya maji
ambayo kwa sasa imepungua baada ya upatikanaji wa maji kufikia asilimia
60.
Akizungumzia mradi wa bwawa hilo alisema
unatarajiwa kunufaisha kata zaidi ya tano kutokana na bwawa hilo kuwa na
uwezo wa kuhifadhi lita 392.04 milioni za ujazo milioni katika kipindi
cha miaka mitatu hata kama mvua hazitanyesha.
Alisema kukamilika bwawa hilo ni sehemu ya mipango
ya Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Maafa waliotoa
Sh3 bilioni .
Mkuu wa wilaya hiyo, Jowika Kasunga alisema
kukamilika kwa bwawa hilo ni utekelezaji wa mipango ya Serikali wa
kuondoa tatizo la maji kwa binadamu na mifugo.
Chanzo Mwananchi
Chanzo Mwananchi
0 comments:
Post a Comment