Home » » UVCCM:VYOMBO VYA ULINZI N USALAMA VIDHIBITI UHALIFUAFRICA MASHARIKI

UVCCM:VYOMBO VYA ULINZI N USALAMA VIDHIBITI UHALIFUAFRICA MASHARIKI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM ) umesema kuchomoza kwa vitendo vya uhalifu katika ukanda wa Afrika Mashariki na matokeo ya milipuko ya mabomu yalioleta maafa katika miji ya Mombasa, Arusha na Zanziabar ni jambo linalohitaji tahadhari ya pamoja ya vyombo vya ulinzi na usalama vya kikanda.
Hayo yalisemwa juzi na Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Binti Amran mjini Unguja.

Alisema vyombo vya ulinzi na usalama vinatakiwa kufanya kazi kwa bidii, ushirikiano na umakini mkubwa ili kuvitokomeza vitendo hivyo mara moja.

Aliviomba vikosi hivyo kujenga umakini na ushirikiano wa karibu katika kipindi hiki kigumu kuliko wakati wowote ili  kufanya kazi kwa pamoja na kuibaini mitandao ya kihalifu katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki.

Hata hivyo, alizitaka Serikali mbili za SMT na SMZ  kuwakabili na kuwaasa viongozi wanaochanganya dini na siasa na kueleza kuwa jambo hilo ikiwa litaachiwa linaweza kuzaa  matatizo na kuleta maafa.

Aidha, alisema kitendo cha kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar si tiketi itakayomsaidia  Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad kushinda na kuwa Rais wa Zanzibar katika  uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.

Shaka alisema si  jambo  jepesi na rahisi kama inavyofikiriwa na baadhi ya viongozi wa CUF wanaoamini kuwa  Maalim Seif atashinda.

Alimtaja  Maalim Seif (pichani)  kama kiongozi aliyepoteza mvuto na  sifa ya kuwa kiongozi wa kitaifa  kutokana na historia yake kuvurugika tokea akiwa Waziri Kiongozi wa SMZ  na baadae kuwa Katibu Mkuu wa CUF kutokana na kusakamwa na  tamaa kushika madaraka kwa  hila na pupa.

Aidha Shaka alimtaja kiongozi huyo kama ni  dikteta wa aina yake kutokana na ung'ang'anizi wake wa  madaraka na kuwa  kiongozi wa kudumu wa CUF tokea mwaka 1992 akikataa kuwapisha wengine.

Alisema kitendo cha kutokaa kwake kando  kuwapisha wenzake kimemvunjia hadhi mwanasiasa huyo na kuonekana mbinafsi, mchoyo na asiyependa kutii miiko ya demokrasia chini ya mfumo wa vyama vingi.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa