Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
DIWANI
wa Levelos, Ephata Nanyaro (CHADEMA) amelitaka Jeshi la Polisi mkoani
Arusha kuacha kufanya kazi kisiasa kwani inaweza kuhatarisha amani na
usalama.
Alidai kuwa siku chache baada ya kutoa kauli kwenye Baraza la
Madiwani akilaani kauli ya kibaguzi ya Mkuu wa Wilaya, John Mongela
aliyedaiwa kuwaeleza machinga wasiotaka kutii kanuni za jiji warudi
walipotoka. Jeshi hilo limemtengenezea kesi ya jinai ya kumpiga mgambo
wa jiji.
Alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari jijini hapa,
kwamba alipigiwa simu juzi (Jumatatu) asubuhi na askari wa upelelezi
aliyejitambulisha kwa jina la Evarest akimtaka afike polisi ili apelekwe
mahakamani pamoja na Naibu Meya, Prosper Msofe (CHADEMA).
Kwa mujibu wa diwani huyo, alibambikiziwa kesi hiyo Aprili 16 mwaka
huu siku waliyopigwa na mgambo kwenye ghala la halmashauri hiyo lililopo
Levelos baada ya wao kufuatilia malalamiko ya wananchi kuwa wanafungiwa
huko na kupigwa na mkia wa faru na kwamba hadi sasa wananchi watatu
wamevunjwa miguu.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment