PICHA NO. 1
Mgeni Rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bi. Evelne Itanisa (katikati) akimsikiliza kwa makini mwakilishi wa Wadau wa Maendeleo (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Namna ya Uandishi Bora wa Taarifa za Kina (Thematic Reports) zinazotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 yaliyonguliwa jana mkoani Arusha. Kulia kwake ni Mkurugeni wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa na kushoto kwake ni Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Said.
PICHA NO. 2
Mgeni Rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bi. Evelne Itanisa akiwahutubia washiriki wa mafunzo ya Namna ya Uandishi Bora wa Taarifa za Kina (Thematic Reports) zinazotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 yaliyofunguliwa jana mkoani Arusha.
PICHA NO. 3
Mgeni Rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bi. Evelne Itanisa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu, Zanzibar pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Namna ya Uandishi Bora wa Taarifa za Kina (Thematic Reports) zinazotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, mafunzo hayo yamefunguliwa  jana mkoani Arusha.
PICHA NO. 4
Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Said akiwa katika mahojiano maalumu na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mafunzo ya Namna ya Uandishi Bora wa Taarifa za Kina (Thematic Reports) zinazotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, mafunzo hayo yamefunguliwa  jana mkoani Arusha.(PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).