Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MAOFISA 50 kutoka idara za takwimu katika wizara, taasisi na vyuo
vikuu vya serikali wanakutana jijini Arusha kupata mafunzo ya jinsi ya
kuchambua takwimu za sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2012 na
kuoanisha na sera mbalimbali za nchi kama zinaendana.
Kukutana kwa maofisa hao kunafanyika siku 14 kabla rais
hajazindua kitabu cha tatu cha taarifa za takwimu zilizotokana na sensa hiyo.
hajazindua kitabu cha tatu cha taarifa za takwimu zilizotokana na sensa hiyo.
Akizungumza na waandishi jana katika ufunguzi wa mafunzo hayo Kamishna
wa Sensa ya Watu na Makazi, Hajati Amina Mrisho, alisema mafunzo hayo
ni muhimu kwa maofisa hao ili kuwawezesha kuandika taarifa za sensa kwa
lugha rahisi zaidi zikiwa zimechambuliwa kwa kina.
“Haya mafunzo ya siku 10 yatahusisha makala 11 zilizoandaliwa kuhusu
Elimu, Afya, Ajira, Vifo, Uzazi na Ndoa na hali ya umaskini katika nchi
ili kusaidia kuoanisha na sera zilizopo kama zinaendana na takwimu
zilizopatikana,” alisema Hajati Amina.
Akionyesha msisitizo katika hilo aliwataka wajumbe kushiriki katika
mafunzo hayo kwa umakini na kasi ili itakapofika siku ya mwisho kila
mmoja atoke na uwezo wa kwenda kuandaa takwimu katika idara yake na
kuziandika kwenye kitabu kitakachotumiwa na idara husika kutengeneza
sera na mikakati mbalimbali.
Alifafanua kuwa matokeo ya uchambuzi wa kina wa Sensa ya watu na
makazi ya mwaka 2012 ni pamoja na kupata viashiria vitakavyowezesha
Tanzania kutathmini na kufuatilia malengo ya Programu za Maendeleo
ikiwemo dira ya maendeleo ya mwaka 2015 kwa Tanzania Bara na 2020 kwa
Tanzania visiwani.
Awali akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo,
aliwasihi washiriki kuwa kipimo halisi cha mafanikio ya mafunzo hayo ni
utoaji wa ripoti hizo kwa wakati na ubora unaotarajiwa.
“Dhamana ya mafanikio haya ipo mikononi mwenu hivyo ni imani ya
serikali kuwa mtatumia juhudi na maarifa ili lengo hilo litimizwe
kikamilifu kwani wadau wanaotegemea taarifa hizo wanazisubiri ili
wazitumie kupanga maendeleo,” alisema Mulongo.
Mafunzo hayo licha ya kufadhiliwa na mashirika ya kimataifa ikiwemo
UNICEF pia yameshirikisha wakufunzi wataalamu kutoka US Bureau of Census
na Havard University vya nchini Marekani kusaidia uboreshaji wa
kuandika takwimu kwa lugha rahisi zaidi kutumiwa na
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment