Home » » WATENDAJI WATAKIWA KUTUNZA VYANZO VYA MAJI

WATENDAJI WATAKIWA KUTUNZA VYANZO VYA MAJI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
MKUU wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego, amewaagiza watendaji wa vijiji, mitaa na kata kuhakikisha wanatunza na kulinda vyanzo vya maji ikiwemo miundombinu yake ili kuwepo na uhakika wa maji.
Dendegu alitoa kauli hiyo jana wakati wa ufunguzi wa semina kwa wenyeviti wa vijiji, mitaa na kata walioko jijini humo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) iliyofanyika Mowe kwenye Kata ya Pande.
Alisema ili huduma ya maji safi na salama iweze kuwa endelevu ipo haja ya kulinda vyanzo vyake na miundombinu isiharibiwe, kwani mabalozi wa karibu ni viongozi hao sababu ndio wapo karibu na wananchi wengi.
 Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa