Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
BENKI ya Exim imezindua tawi mjini Arusha linalolenga kuwahudumia wateja wake wakubwa ndani ya mkoa huo na maeneo ya jirani.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi hilo mwishoni mwa wiki,
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Yogesh Manek alisema
tawi hilo jipya linadhihirisha jitihada za benki kutoa huduma bora kwa
wateja wake wote.
“Tawi letu hili lakipekee litatumika kuhudumia wateja wetu wakubwa na
kukidhi matakwa yao kikamirifu kwa kutoa huduma zote za kibenki za
kipekee katika eneo maalum… jitihada hizi zinaenda na dhamira ya Benki
ya Exim ya kutoa huduma bora katika sekta zote,” alisisitiza.
Manek alisema tawi hilo lina wataalam wa kutosha waliotayari kutoa
fumbuzi wa masuala ya kibenki huku akisisitiza kwamba benki yake
imejikita katika mkakati unaolenga kuiwezesha benki hiyo kuongoza kwa
utoaji wa huduma bora za kifedha Tanzania.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment