Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
ASASI ya wakulima wa mazao ya maua na mbogamboga nchini (TAHA)
na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), linalofadhili Mpango wa
Uzalishaji wa Kilimo Tanzania (TAPP), zimekubaliana kuanzisha vituo vya
mafunzo ya kilimo cha mazao hayo kwa kushirikiana na wadau wengine wa
sekta za umma na binafsi.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini hapa jana, Mkurugenzi Mtendaji
wa TAHA, Jacqueline Mkindi, alisema mpango huo unatarajiwa kutoa
matokeo mazuri kwa wadau wa kilimo cha mazao ya maua na mboga mboga
nchini.
Mkindi alibainisha hivi sasa wapo katika mchakato wa uanzishaji wa
vituo hivyo ambapo utahusisha taasisi za serikali za utafiti na mafunzo
kama vile Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Taasisi ya Utafiti
Uyole mkoani Mbeya, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo cha Mazao ya Maua na
Mboga mboga (HORTI-Tengeru), na Kituo cha Utafiti cha Kizimbani
Zanzibar katika kuanzisha vituo vya mafunzo ya kivitendo (PTCs).
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment