Home » » SERIKALI YAMTULIZA MWEKEZAJI MZAWA

SERIKALI YAMTULIZA MWEKEZAJI MZAWA

SERIKALI imemtoa hofu mwekezaji mzawa,Philemon Mollel wa kampuni ya Monaban ya jijini Arusha kuhusu ombi lake la kutaka kuuziwa mali zilizokuwa za shirika la usagishaji la Taifa (NMC) mkoani hapa, ambapo kwa sasa amewekeza

Akizungumza baada ya kutembelea mali za shirika hilo,waziri wa kilimo,chakula na ushirika,mhandisi Christopher Chizza,alisema kuwa mchakato wa uuzwaji wa mali za shirika hilo utaamuliwa na baraza la mawaziri baada ya kujiridhisha kwamba anastahili kuuziwa mali hizo.

Waziri Chiza amesema kuwa kwa sasa hawezi kutoa jibu la moja kwa moja ila alimtaka Mollel aendelee na shughuli zake za usagishaji kwani serikali imeridhishwa na mipango yake ya kuendeleza kinu hicho na kuendelea kuhudumia jamii ikiwemo mpango wake wa kujenga maghala zaidi ya kuhifadhi nafaka kwa wakulima.

Amesema kampuni ya Monabani iliomba kuuziwa Kinu hicho kilichopo Arusha kutokana na kufanya vizuri kwa uzoefu na kukiendeleza ,hata hivyo alisema serikali iliamua kukabidhi mali zilizobaki kwenye bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko zikiwemo za Iringa na kubakia za mkoani Arusha.


Awali Mkurugenzi wa kampuni ya Monaban Philemon Mollel amesema kuwa kampuni yake imewekeza kwa muda mrefu kwa mtaji wa zaidi ya shilingi bilioni 6,hivyo haoni sababu ya kutouziwa kinu hicho ama kubinafisishiwa kwa asilimia 100.

Amesema kampuni yake inamkakati wa muda mrefu na mfupi ambapo mkakati wa muda mfupi ni kuanzisha mradi wa kutengeneza juisi , maji safi na salama ya kunywa ,kuoka mikate yenye ubora hatua ambayo itasaidia kuimarisha ajira kwa wananchi.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa