Home » » Nyalandu: Nitataja majina 320 wahusika wa ujangili

Nyalandu: Nitataja majina 320 wahusika wa ujangili

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu.
 
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu amesema wakati wowote kuanzia sasa atataja majina ya watu  320 waliohusika katika masuala ya ujangili wa meno ya tembo.
Nyalandu alisema hayo jana katika mahojiano maalum na NIPASHE Jumamosi, wakati wa uzinduzi wa kituo cha Utamaduni kitakachohusika na utunzaji wa majengo ya zamani.

Mradi huo, unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa Uro milioni saba, sawa na bilioni 14.

Nyalandu alisema kukamatwa kwa watu hao, ni jitihada zilizofanywa na serikali na kwamba miongoni mwao wamo Watanzania na wengine kutoka nje ya nchi.Watu hao ni wale waliotiwa mbaroni kati ya 2012 na 2013.

Alisema Alhamisi ya wiki hii alikutana na mawaziri wa utalii wa nchini Kenya na Uganda mjini Arusha pamoja na mambo mengine walizungumzia jinsi ya kujidhatiti na ujangili.

“Tumezungumzia jinsi ya kujidhatiti kwenye mipaka ya nchi zetu hasa viwanja vya ndege na upande wa bahari,” alisema.

Pia alisema wale vigogo 40 ambao Rais Jakaya Kikwete aliowazungumzia walitiwa mbaroni mwezi Mei mwaka jana na kwamba hatua hiyo ilitokana na serikali kufuatilia mienendo yao na kubainika kujihusisha na picha zao zipo.

Alisema watu hao walikamatwa kupitia operesheni maalum ya kikosi kazi inayoendeshwa kati ya jeshi la polisi, Idara ya wanyamapori na Usalama.

Hata hivyo, alisema vigogo hao ambao walitajwa na Rais Kikwete imetokana na operesheni ya kanda hiyo ya Kaskazini na kwamba zipo operesheni kwenye kanda nyingine zinaendelea.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa