JAJI Mstaafu Agustino Ramadhani amesema kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba wanatakiwa kuzingatiaza uzalendo kwanza,na badala yake waachane na kutaka kuongezewa posho ambazo wanadai hazitoshi kutokana na kupanda kwa gharama za maisha kama ilivyoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini.
Jaji Ramadhani ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati akifungua Mkutano wa chama cha Wanasheria Tanzania (TLS),ambapo alisema suala la posho ya Wajumbe wa Bunge la Katiba kulipwa kiasi cha laki tatu 300,000 ni kiasi ambacho ni kikubwa kwa Watanzani walioajiriwa na waliojiajiri hawaingizi hiyo hela kwa siku hivyo amewataka waone ni heshima kubwa waliyopewa.
Naye raisi wa Chama hichoFrancis Stola alisema kazi ya Bunge la Katiba itapimwa na wananchi kupitia kura ya maoni ya Katiba inayowapa mamlaka ya kuikataa katiba hiyo au kuikubali kama itaonekana maoni yao hayakuzingatiwa.
Amesema kuwa kiwango cha madaraka ya Bunge la Katiba hakijaainishwa wazi na sheria hiyo ,hivyo katiba watakayoipendekeza itarudishwa kwa wananchi ambao ndio wana mamlaka na kukubali itumike kwa manufaa ya nchi aua la!
Wakati maombi ya baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba ya kutaka kuongezewa posho yakipingwa kila kona, uongozi wa muda wa Bunge hilo juzi uliunda kamati kuchunguza uhalali wa maombi hayo.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment