Home » » Karatu kuundiwa mamlaka

Karatu kuundiwa mamlaka

Serikali imetangaza mpango wa kuunda, Mamlaka ya Maji, katika mji wa Karatu.
Mpango huo ulitangazwa juzi na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Profesa Maghembe alisema, baada ya kukamilika kwa Mradi wa Maji wa Karatu, unaotarajiwa, kuwanufaisha asilimia 81 ya watu, Serikali itaunda Mamlaka ya Maji Karatu.
“Tunawapongeza sana Mamlaka ya Majisafi na Maji taka Arusha (Auwsa), kwa kukamilisha kwa wakati mradi huu na sasa maji yameanza kutumika na kazi inayofuata ni kuwana mamlaka,” alisema Profesa Maghembe.
Alisema mamlaka hiyo, itakuwa na jukumu la kusimamia mradi huo ikiwa ni pamoja na kupanga bei ya maji ili mradi uwe endelevu.
Alisema mamlaka hiyo, itaundwa kwa kutumia sheria ya maji
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa