Home » » BUNGE LA KATIBA LITAPIMWA NA WANANCHI - TLS

BUNGE LA KATIBA LITAPIMWA NA WANANCHI - TLS

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Na woinde shizza,Arusha

Raisi wa Chama cha Wanasheria Tanzania ,Tanganyika Law Society (TLS),Francis Stola amesema kuwa kazi ya Bunge la Katiba itapimwa na wananchi kupitia kura ya maoni ya Katiba inayowapa mamlaka ya kuikataa katiba hiyo ama kuikubali endapo wanaona kuwa maoni yao hayakuzingatiwa.

Licha ya kifungu cha 25 cha sheria ya mabadiliko kutokufafanua madaraka halisi ya tume hiyo lakini pia wametakiwa kutengeneza katiba inayotakiwa na Watanzania walio wengi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Mkutano wa chama hicho ,Stola amesema kuwa kiwango cha madaraka ya Bunge la Katiba hakijaainishwa wazi na sheria hiyo na hata hivyo katiba watakayoipendekeza itarudishwa kwa wananchi ambao ndio wana mamlaka kamili katika kuipigia kura ipitishwe ama isipitishwe.

“Wananchi wakiona maoni yao hayamo wanaruhusiwa kuikataa ,tunaamini madaraka ya Bunge la Katiba hayataathiri maoni ya wananchi kwasababu Rasimu ya pili ya Katiba imejengwa na Sauti za watanzania na maoni yao pia ” Alisema Stola.

Kwa upande Jaji Mstaafu Agustino Ramadhani amesema kuwa Bunge la Katiba lina mipaka haliwezi kubadilisha kila kitu ni kuinoa tu. “Msimamo wa tume umeshatolewa na na Mwenyekiti Jaji Warioba ,maoni yangu ni kwamba Wajumbe Waangalie maslahi ya Tanzania tunayoitaka wasiangalie misimamo ya vyama” Alisema Warioba.

Pia amezungumzia suala la posho ya Wajumbe wa Bunge la Katiba na kueleza kuwa malipo hayo ya kiasi cha laki tatu 300,000 ni kiasi ambacho ni kikubwa kwa Watanzani walioajiriwa na waliojiajiri hawaingizi hiyo hela kwa siku hivyo amewataka waone ni heshima kubwa wamepewa kwa kufanya jambo k wa mustakabali wa taifa na hakuna anyeweza kuwalipa kwa kazi hiyo.

Naye Raisi wa Shirikisho la Wanamuziki Tanzania ,Ado Novemba Masongo akizungumzia suala la posho ya wajumbe wa bunge hilo amesema kuwa suala hilo ni fedheha na wamesikitishwa sana na jambo hilo kwani walipaswa kugharamiwa na taasisi walizotoka ili kulifanya jambo hilo kwa uhuru zaidi.

“Inasikitisha sana kuna walimu mishahara yao haifiki laki 3 kwa mwezi,polisi na wanajeshi lakini wao wanaitaka kwa siku moja,wameonyesha makucha yao mapema tuko tayari kuandaa maandamano tukishirikiana na wananchi kupinga suala hili” Alisema Ado
Chanzo: Michuzi Media Group

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa