Arusha
Home » » KAMPUNI YA MEGATRADE YATOA MSAADA WA VYAKULA KWA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU JIJINI ARUSHA

KAMPUNI YA MEGATRADE YATOA MSAADA WA VYAKULA KWA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU JIJINI ARUSHA


DSCF1881Wafanyakazi wa kampuni ya  Megatrade wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo cha New Paradise kilichopo kata ya sokoni 1 jijini Arusha,wakionekana wenye furaha kabisa baada ya kukabidhiwa msaada huo wa vyakula mbalimbali kwa ajili ya kusherehekea sikuu ya krismasi na mwaka mpya .DSCF1874Meneja mauzo na masoko Goodluck Kway wa kampuni ya Megatrade  Investment akiwa anamkabidhi mmoja wa watoto yatima  katoni ya soda (mwenye T-shirt ya blue) ikiwa ni sehemu ya kuwapa matumaini mapya watoto hao waishio katika mazingira magumu,msaada huo wa vyakula mbalimbali umetolewa kwenye kituo hicho kwa ajili ya sikuu ya krismasi na mwaka mpya.DSCF1869Sehemu ya baadhi ya vitu vilivyotolewa na kampuni ya Megatrade  Investment kupitia kinywaji chake cha K-vant Gin katika kituo cha watoto yatima cha New Paradise kilichopo kata ya sokoni 1 jijini Arusha kwa ajili ya kusherehekea Krisimasi na mwaka mpya.
Na Pamela Mollel,Arusha
KAMPUNI ya Megatrade Ivestment kupitia kinywaji chake cha K-vant Gin imetoa misaada  ya vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu  kwaajili ya sikukuu ya krismasi na mwaka mpya katika kituo cha New Paradise kilichopo kata ya sokoni 1 jijini Arusha
Akikabidhi msaada huo juzi  kituoni hapo Meneja mauzo na masoko Goodluck Kway wa kampuni ya hiyo kupitia kinywaji chake cha K-vant Gin alisema utowaji wa misaada kwa makundi maalum yenye uhitaji ni utaratibu wao wa kurudisha faida waliopata kwa mwaka mzima kwa jamii
Alisema msaada huo walioutoa umegharimu kiasi cha  shilingili Milioni moja, ambapo watoto hao watasherehekea sikukuu kama watoto wengine, huku akitoa rai kwa makampuni kujitokeza kuwasadia watu wenye uhitaji wa namna mbalimbali.
Misaada iliyokabidhiwa kituoni hapo ni pamoja na sukari,mafuta ya kula,mchele,katoni za soda,sabuni,kalamu,madaftari,unga wa ugali,unga wa ngano na maziwa.Mlezi mkuu wa kituo hicho Christopher Kaaya alisema kampuni hiyo imekuwa msaada mkubwa kwao na amewaomba waendelee na moyo huo  wa kuwasaidia
“Mungu awazidishie sana kwa sababu wamekuwa watu wa karibu kwetu hata siku ya kwanza  walituchangia katika ujenzi wa jengo hili na pia kila mwaka lazima watuletee zawadi za chrismasi na mwaka mpya”alisema Kaaya
Kituo hicho kinajumla ya watoto 24 wasichana wakiwa 14 na wavulana 10 ambapo idadi imeongezeka ukilinganisha na mwaka jana watoto walikuwa 20 tu kituoni hapo.
Chanzo;Michuzi blog

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa