Na Gladnesss Mushi, MERU
CHAMA
cha Mapinduzi Wilaya ya Meru Mkoa wa Arusha kimeweka utaratibu maalumu
wa kuhakikisha kuwa kinashirikiana na taasisi mbalimbali za fedha ili
kuweza kutoa elimu pamoja na huduma mbalimbali za kifedha hasa maeneo ya
vijijini huku lengo likiwa ni kuongeza ufanisi wa kiuchumi
Hayo
yamelezwa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Chama hichoBw Furaini Mungure
wakati akiongea na wananchi wa Mareu kuhusiana na umuhimu wa kujiunga na
taasisi za fedha
Mungure
alisema kuwa mpango huo utaanza hivi karibuni na utafadhiliwa na chama
hicho ambapo taasisi hizo zitaitwa na kisha kuanza kutoa elimu juu ya
masulaa mbalimbali ya kifedha
Alifafanua
kuwa mpango huo utaenda katika maeneo ya vijijini zaidi ambapo mpaka
sasa takwimu zinaonesha kuwa pamoja na kuwepo kwa huduma nyingi za
kifedha katika maeneo ya mijini lakini vijijini bado wananchi wengi
hawajui hata umuhimu wa kutumia huduma hizo
Mbali
na hayo alidai kuwa kwa sasa kuna umuhimu mkubwa sana wa Mabenki nayo
kujiwekea utaratibu wa kutoa elimu ya masuala mbalimbali kama vile
ukopaji hasa vijijini kwani wengi sana wanaokopa huishia kwenye
mashindano ya nguo lakini hata Vinywaji
Alisema,kama
wananchi watapata elimu ya kutosha hususani kwenye suala zima la
ukopaji ni wazi kuwa mikopo inayotolewa katika maeneo ya vijiji itaweza
kusababisha mabadiliko ya uchumi lakini pia hata idadi ya wakopaji nayo
itaongezeka sana.
0 comments:
Post a Comment