MKUU wa Chuo cha Uhasibu, Profesa Johannes Monyo, amewataka
wahitimu kuacha kusubiri kuajiriwa na badala yake kuwa wabunifu wa
kutosha wa kutengeneza au kutafuta fursa.
Profesa Monyo alitoa wito huo hivi karibuni wakati alipozungumza na wahitimu wa shahada ya uzamili.
Alisema itashangaza kukuta wasomi kama wao wakikaa vijiweni
wakilalamikia ukosefu wa ajira nchini bila kutumia elimu aliyoipata
kubuni njia sahihi za kumuwezesha kupata fursa za ajira.
Alisema chuo hicho hivi sasa kimeendelea kujitanua ambapo tayari
kimefungua tawi lake jijini Dar es Salaam na kina mpango wa kufungua
tawi kama hilo jijini Mwanza ili kusaidia idadi kubwa ya Watanzania
kupata elimu.
Naye Mkuu wa Kitivo cha Uhandisi na Kompyuta, Chuo Kikuu cha Coventry
cha Uingereza (CU), Barbara Howell, amewataka wasomi wa Tanzania
kutumia kwa vitendo elimu waliyoipata waweze kuleta mabadiliko katika
maeneo yao.
Howell, ambaye ndiye aliwatunukia shahada wahitimu hao kwa niaba ya
Chuo cha Coventry, ambacho kina ushirikiano na Chuo cha Uhasibu katika
kuendesha mafunzo hayo kwa ngazi ya shahada ya uzamili aliwasihi
kulisaidia taifa la Tanzania kupitia elimu waliyoipata.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment