Home » » Chadema yawazungumzia Zitto, Lema

Chadema yawazungumzia Zitto, Lema

Freeman Mbowe
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kimesema sakata la  mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema na Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, ni malumbano ya kawaida ya viongozi kutofautiana kimawazo.
Mkurugenzi wa Oganizasheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kilichojiri kwenye mkutano wa Kamati Kuu (CC)unaoendelea jijini Dar es Salaam.

Alisema suala hilo litajadiliwa kwenye kikao hicho na taarifa itatolewa na mwenyekiti, Freeman Mbowe, (pichani chini).

Kigaila aliongeza kuwa ajenda zilizojadiliwa ni hesabu zilizokaguliwa na zilizopelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa, yatokayo na vikao viwili vya  dharura vya CC, upangaji upya wa kurugenzi ya chama makao makuu na nguvu kazi ili kutekeleza majukumu vizuri.

Nyingine ni uundaji na ujenzi wa chama ngazi za chini ambazo ni msingi wa chama na kwamba kwa sasa wanajadili kanda ya ziwa mashariki yenye mikoa ya  Mara, Shinyanga, na Simiyu yenye majimbo 19 na wapiga kura ,milioni 1.7

Alisema ajenda ya mwisho itahusu hali ya kisiasa ndani na mahusiano ya kimataifa.

Alisema suala la aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, halitajadiliwa kwa kuwa mamlaka ya nidhamu ya kanda yake na kama atapenda kukata rufaa ndipo lingeweza kujadiliwa na hadi sasa hajafanya hivyo.

 
CHANZO: NIPASHE



0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa