Utata
umegubika kuhusu hali ya majeruhi Violeth Mathias aliyepigwa risasi na
polisi kwa madai ya kuwatishia bastola, baada ya Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, kukataa kuzungumza na waandishi wa
habari kuhusu tukio hilo kama alivyoahidi, huku uongozi wa Hospitali ya
Rufaa ya Selian ukiwawekea ngumu waandishi wa habari kumwona na
kuzungumza naye.
Pamoja na taasisi hizo kukataa kutoa taarifa za maendeleo ya majeruhi huyo, Violeth mwenyewe naye alikataa kuonana na waandishi wa habari kuzungumzia tukio lililomjiri.
Katibu muhtasi wa ofisi ya Utawala hospitalini hapo alipiga simu mapokezi kutoa taarifa kwamba mgonjwa hataki kuonana na waandishi wa habari, simu ambayo ilipokelewa na mwandishi wa habari mmoja.
Lakini taarifa zilisema majeruhi alikwishafanyiwa upasuaji.
Mapema majira ya saa 3:30 asubuhi, waandishi wa habari walifika hospitalini hapo na kuwasiliana na uongozi wa hospitali, lakini walielezwa madaktari wameingia chumba cha upasuaji hivyo wasubiri mapokezi watakuja kuchukuliwa na mtu wa kuwapeleka kwa mgonjwa.
Wakati waandishi wakisubiri majira ya saa 4.15 alitokea Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Akili Mpwapwa, akiwa amevaa kiraia akaomba kwenda kumsalimia majeruhi na hapo baadhi ya waandishi walijiunga pamoja naye lakini waligonga mwamba walipofika mlango wa chumba alicholazwa baada ya kutakiwa kutoa kitambulisho na walipobaini ni vya waandishi wa habari walizuiwa.
Alifika akiwa na gari la polisi, na kuruhusiwa kumwona mgonjwa, lakini alitakiwa kutoa kitambulisho alipofika mlango wa chumba cha mgonjwa.
Ulinzi ulikuwa umeimarishwa eneo la mapokezi na katika chumba alikolazwa, hivyo kuwafanya waandishi wa habari wazuiwe kuingia na kumwona majeruhi.
Mwandishi aliyeambatana na RPC Mpwapwa na kuzuiwa mlangoni, alisema kulikuwa na mlinzi mmoja wa kike aliyekuwa akitaka vitambulisho kwa kila mtu aliyekuwa akitaka kuingia chumbani humo tofauti na vyumba ambavyo walikuwa wamelazwa wagonjwa wengine.
Baada ya kuzuiwa, waandishi walikwenda kuonana na Kamanda Sabas, ofisini kwake majira ya saa 5:00, lakini alidai kuwa anaumwa na hivyo hawezi kuzungumzia tukio hilo.
Baada ya majibu hayo, waandishi wa habari waliamua kumpigia simu Mkuu wa Mkoa Arusha, Magesa Mulongo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, aweze kutoa maelezo ya tukio hilo.
Hata hivyo, Mulongo alikataa ktoa ufafanuzi na kuamua kukata simu.
Violeth alipigwa risasi juzi na polisi waliokuwa wakilinda Benki ya CRDB tawi la Mapato jijini hapa, baada ya kuegesha gari lake kwenye lango la kuingilia ndani linalotumiwa na magari kwenda kuchukua fedha au kupeleka fedha benki.
Inadaiwa Polisi walimzuia asiliegeshe, lakini alikataa na kuingia ndani benki hali ambayo iliwalazimu walitoe upepo matairi yote.
Baada ya kutoka ndani ya benki na kuona gari lake likiwa limetolewa upepo matairi, alianza kujibizana na polisi na kisha akawatolea bastola na ndipo polisi walipomuwahi kwa kumpiga risasi begani.

CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment