Mkuu wa Mkoa Arusha,Magesa Mulongo
Aliyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa siku ya wadau wa Mfuko wa Bima ya Afya mkoani humu mwishoni mwa wiki.
Alisema anasikitishwa kuona madaktari wa siku hizi wanatanguliza fedha mbele kwa kulazimisha wagonjwa kuwapatia posho kabla ya kuwahudumia, hali ambayo tofauti na zamani, walikuwa wakitoa huduma kwanza ili kuokoa maisha ya mgonjwa.
“Sasa kama daktari au mhudumu anadai posho kabla hata ya kuokoa maisha ya mgonjwa, hii siyo hatari na hii inakwamisha ongezeko la wateja wa bima,” alisema Mulongo.
Akitoa mfano kwa Mkoa wa Arusha, Mulongo alisema ni waathirika wakubwa wa kauli mbaya kwa wagonjwa.
"Mkoa una wakazi zaidi ya milioni 1.5, lakini waliopo katika Mfuko wa Bima ya Afya ni ndogo sana sawa na asilimia 2.2, hiyo ina maana watu asilimia 98.8 hawako katika utaratibu huo.
Naye mjumbe wa Bodi ya Mfuko huo kutoka makao makuu, Raphael Chegeni, alisema kwa sasa watoa huduma hawatendi haki kwa wagonjwa wao kwani huwalazimisha kusaini fomu za malipo kabla ya kuwapatia huduma na kuongeza madai nje ya huduma za mgonjwa alizopata.
“Unakuta mgonjwa ametibiwa jipu na baadaye kwa kuwa amesaini fomu, anabambikiziwa fedha nyingi kinyume na huduma halisi. Sasa hatutalipa kabisa madai yasiyo halali,” alisema Chegeni.
Pia alipiga marufuku kwa wateja wanaotumia vitambulisho vya bima kuwapa wenzao ili wapate huduma.
Chegeni alisema kufanya hivyo sawa na wizi kwa mfuko huo na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment