Mbunge wa Arusha, Godbless Lema, ameendelea kushikilia madai yake
kuwa polisi wanahusika na tukio la bomu lililolipuka katika mkutano wa
kampeni ya chama hicho Viwanja vya Soweto Arusha na kusababisha vifo vya
watu wanne.
Lema alitoa madai hayo juzi alipohutubia mkutano wahadhara Viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro.
Alidai Rais Jakaya Kikwete amegoma kuunda tume huru ya kimahakama
kuchunguza tukio hilo, ili kunusuru polisi na aibu ya kushiriki uhalifu
na mauaji ya raia wasio na hatia.
“Mauaji ya Soweto yalipangwa na kutekelezwa na polisi, RPC (Kamanda
wa Polisi) wa Arusha anajua mpango mzima ndiyo maana Rais hataki kuunda
tume kama Chadema tulivyomuomba, ili tuwasilishe ushahidi wa video
kuonyesha jinsi walivyohusika,” alisema Lema
CHANZO VIJIMAMBO BLOG
0 comments:
Post a Comment