Picha
ya juu ni
trector iliyotengenezwa na mkulima mbunifu wa Meru-Arusha anayefahamika
kwa jina la
Justin Mungure. trector hii ameipa jina la "LUKUA-SI" ambapo maana
yake ni chimbua ardhi. Trector hii aliitengeneza kwenye karakana yake
mwaka 2012 kwa kutumia engine ya pikipiki yenye 125cc. Trector hii
ina uwezo wakulima hekari tatu kwa siku ambapo hutumia kiasi cha lita
tatu tu za mafuta ya petrol kwa heka moja. Mgunduzi huyu ameshaifanyia
trector
hii utafiti wa miezi mitano na imeonyesha ufanisi mkubwa kwa wakulima
wadogowadogo. "Niliamua kubuni na kutengeneza trector hii inayotumia
engine ya pikipiki baada ya kuona kuwa mkulima mdogo hana mtu
anayemjali. Kazi ya kulima na kuzalisha mazao ni ngumu japo ni muhimu" alisema Justin Mungure. Pia aliendelea kusisitiza kuwa
anaomba serikali iwathamini wagunduzi wa ndani na kuwawezesha ili
waweze kufikia malengo yao maana anaamini wapo watanzania wenye uwezo
mkubwa sana wa kubuni na kutengeneza vitu mbalimbali na vyenye kuweza
kuleta faida kubwa kwa taifa kama walivyo wagunduzi wengine wa nje ya
nchi. kwa mawasiliano ya mgunduzi huyu 0754 842 219
Maonesho
ya nane nane yameanza tarehe 1/08/2013 na yataendelea hadi tarehe
10/08/2013. Lengo la
maonesho haya ni kuwapa wakulima na wafugaji wa Tanzania fursa ya kuweza
kuonesha utaalamu walionao katika kuzalisha bidhaa mbalimbali. Ujumbe
wa
mwaka huu ni "Zalisha kwa kuzingatia mahitaji ya soko"
CHANZO KILIMANJARO OFFICIAL BLOG
0 comments:
Post a Comment