Na Leonce Zimbandu
Mkoa wa
Arusha umetajwa kuwa umeongoza katika udanganyifu na wizi wa mitihani
kwa asilimia 48 kati ya asilimia 61 ya wanachama 31 wa Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi wa shule za msingi.
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa shule na Vyuo visivyo vya
Serikali (Tamongsco), Benjamin Nkonya, alitoa kauli hiyo jana kwa
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Alisema
wizi wa mitihani ni saratani inayotafuna ubora wa elimu nchini, kamwe
hali hiyo ikiendelea upo uwezekano wa Taifa kutumbukia kwenye umaskini
wa kukosa uelewa na kushindwa kupata maendeleo ya kweli ya kiuchumi.
Nkonya
alisema Tamongsco ina uhakika kwamba maendeleo ya kweli ya uchumi
yanapatikana kwa kuboresha elimu, lakini kwa udanganyifu uliojitokeza wa
mitihani ni ndoto maendeleo hayo kupatikana.
“Wizara
ya elimu imetuarifu rasmi kuwa Mkoa wa Arusha ni kinara wa wizi na
udanganyifu wa mitihani, ukifuatiwa na Kagera kwa asilimia 13, Dar es
Salaam na Mara asilimia sita na mikoa mingine uliyobaki ina asilimia 3
kila mmoja,” alisema.
Chanzo: Nipashe
0 comments:
Post a Comment