Home » » TBL YAZINDUA KINYWAJI KIPYA CHA FARU DARK LAGER

TBL YAZINDUA KINYWAJI KIPYA CHA FARU DARK LAGER

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kwa mara nyingine imezindua bia yenye hadhi ya kimataifa ya Faru Dark Lager. Akizungumza mjini hapa jana wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Faru Dark Lager, Kabula Nshimo, alisema bia hiyo itasambazwa kwa wateja wa Kanda za Kaskazini Mashariki na Kaskazini Magharibi.

Alisema bia hiyo imetengenezwa kwa utaalamu wa hali ya juu, huku ikiwa na utofauti wa kipekee katika muonekano na ladha yake.

“Bia hii mpya inajulikana kwa jina la Faru Dark Lager, ni bia inayotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu, inayoifanya kuwa laini na rahisi kunywa, ina kilevi cha asilimia 5.2.

“Baada ya uzinduzi katika kanda hizo mbili, Faru itasambazwa nchi nzima. Tunaamini bia hii italeta mapinduzi makubwa katika soko la vileo hapa nchini,” alisema Kabula.

Alisema bia hiyo inauzwa kwa Sh 1,800 kwa chupa moja kwa bei ya rejareja na itawapa fursa wadau na wapenzi wa bia kuipata kwa urahisi.

“Tumeipa bia hii jina adhimu la mnyama Faru kwa ajili ya kumuenzi mnyama huyo mwenye nguvu, mvuto na thamani ya kipekee. Tuna imani kubwa kuwa wapenzi wa bia wataifurahia Faru Dark Lager,” alisema Kabula.
Chanzo: Mtanzania

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa