
KOCHA ALI MTUMWA, MKURUGENZI WA ROLLINGSTONE ACADEMY

WACHEZAJI WA TIMU YA ROLLINGSTONE WAKIWA MAZOEZINI KATIKA UWANJA WA SHEIKH AMRI ABEID JIJINI ARUSHA

KOCHA ALI MTUMWA AKITOA MAELEKEZO KWA WACHEZAJI WAKE
(Picha na Idd Uwesu Arusha yetu blog)
Na Idd Uwesu Arusha yetu
Wakati michuano ya soka ya Rollingstone inayoshirikisha nchi za Afrika Mashariki na kati yanakaribia timu ya kituo cha Rollingstone jijini Arusha imeendelea kujinoa katika uwanja wa sheikh Amri Abed ili kuhakikisha inafanya vizuri katika michuano ya mwaka huu.
Hali hiyo inatokana na kituo hicho kutofanya vizuri katika michuano ya mwaka jana inayoshorikisha timu za vijana walio chini ya umri wa miaka 20.
Akizungumza na Arusha yetu blog katika uwanja wa Sheikh Amri Abedi Jijini Arusha Kocha wa Rollingstone ambaye pia ni rais wa taasisi ya kuibua na kukuza vijana ya Rollingstone Ali Mtumwa amesema maandalizi yanalenga kurekebisha kasoro zilizojitokeza mwaka jana ili kfanya vizuri katika michuano hiyo amabya mwaka huu inafanyika nchini Burundi.
Aidha amesema kuwa mfumo wa uandaaji wa timu za vijana inabidi uangaliwe upya kwa lengo la kupata wachezaji wenye sifa na uwezo mzuri wa kusakata soka na kuwa msaada kwa timu ya taifa lakini pia kuhakikisha soka la Tanzania linakua.
Kwa upande mwingine kocha huyo ameongeza kuwa ili kupata timu ya taifa itakayoweza kuiwakilisha Tanzania ni vyema maandalizi yaanze mapema kwa kuzishirikisha academies mbalimbali ambazo kimsingi ndio chimbuko la kupata wachezaji bora ikiwa na sambamba na kuzitengenezea mazingira yatakayoziwezesha kufanya kazi nzuri kama kuzisaidia vifaa vya mazoezi na mahitaji mengine muhimu kwa wachezaji
Mtumwa amewataka wadau wa soka, serikali na taasisi zisizo za kiserikali kuzipiga jeki academy za hapa nchini.
Michuano ya Rollingstone ambayo hufanyika kila mwaka jijini Arusha,mwaka huu imepangwa kufanyika nchini Burundi huku ikishirikisha timu kutoka Kenya, Uganda, Rwanda Congo DRC na Tanzania, ambapo timu zote zilizoshiriki mwaka jana zimethibitsha kushiriki isipokuwa timu ya TSC Sports Academy ya Mwanza inayokwenda Ujerumani kushiriki michuano maalum.
0 comments:
Post a Comment