Home » » MAFUNZO KWA WATOA DAWA ARUSHA‏

MAFUNZO KWA WATOA DAWA ARUSHA‏

Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa makini

 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dr. Frida Mokiti akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo
.Meneja TFDA kanda ya kaskazini Damas Matiko
Picha na Idd Uwesu Arusha yetu

*********************
Na Idd Uwesu Arusha yetu
Mamlaka ya dawa na chakula TFDA imeandaa mafunzo maalum kwa watoa dawa wa jijini Arusha yenye lengo la kuwapa utaalamu na uwezo zaidi wa kutoa madawa hayo kwa wagonjwa na kuyapandisha maduka ya dawa baridi hadi kuwa maduka ya dawa muhimu.
Mafunzo hayo ambayo yanawahusisha madaktari wasaidizi, wauguzi na watoa huduma za madawa katika maduka ya dawa yanaendeshwa chini ya mpango wa wizara ya afya kupitia Mamlaka ya dawa na chakula na shirika lisilo la kiserikali la Sayansi ya Usimamizi wa Afya (MSH)
Akifungua rasmi mafunzo hayo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dr. Frida Mokiti amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia kwa makini kile watakachofundishwa na wakufunzi wao ili kuhakikisha lengo la mafunzo hayo linatimia na kuwa suala utoaji dawa limekuwa na changamoto hivyo wao kama wanafunzi wanapaswa kumaliza mafunzo hayo wakiwa wameiva.
Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Chakula kanda ya kaskazini Damas Matiko amesema baada ya utafiti uliofanywa na kubaini mapungufu yaliyopo katika sekta hiyo ndiyo hasa sababu iliyofanya serikali kuona sababu ya kuandaa mafunzo haya.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru serikali kwa kuwaleta mafunzo haya na kuongeza kuwa yataboresha zaidi utendaji kazi na hivyo kuwawezesha kufanya kazi kwa ueledi.
Mafunzo hayo yatatolewa kwa muda wa mwezi mmoja huku yakihusisha halmashauri sita za mkoa wa Arusha.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa