
Katibu mtendaji TATO, Mustapha Akunaay akiongea na waandishi wa habari

Mjumbe wa kamati ya maandalizi Andrew Malalika

Baadhi ya mabanda katika uwanja wa Magereza yakiwa tayari kwa kazi
Na Idd Uwesu- Arusha Yetu
******************
Maonesho ya kimataifa ya Karibu Trade Fair yanatarajiwa kuzinduliwa ijumaa hii huku Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyarandu akitarajiwa kuyazindua rasmi jijini Arusha
Maonesho hayo ambayo ni ya 12 na yaliyokuwa yafanyike mwishoni mwa mwezi wa tano na kuahirishwa ili kupisha Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika yatafanyika katika viwanja vya Magereza jijini humo.
Akiongea na waandishi wa habari katibu mtendaji wa chama cha watoa huduma za utalii Tanzania TATO ambao ndio waandaaji wa maonesho hayo Mustapha Akunaay, amesema maandalizi kwa ajili ya maonesho hayo yamekamilika kwa kiasi kikubwa huku wakiwa wamefanya maboresho makubwa ya miundo mbinu na huduma muhimu uwanjani hapo.
Ameongeza kuwa maonesho haya ambayo ni ya pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya yale ya Indaaba ya Afrika kusini, mwaka huu yamepata washiriki wapya kutoka nchi za brazil, Norway na china.
Nae mjumbe wa kamati ya maandalizi Andrew Malalika amesema bonanza linalohusisha michezo mbalimbali ambalo huandaliwa sambamba na maonesho hayo litafikia tamati siku ya ijumaa katika viwanja vya General tyre vilivyoko Njiro jijini hapa na kuongeza kuwa michezo mbalimbali itahusishwa ikiwemo mpira wa miguu, kuvuta kamba na kukimbiza kuku.
Maonesho hayo yanayofanyika kila mwaka yana lengo la kuwakutanisha wadau wa sekta utalii nchini na wale wanouza utalii kutoka nje ya nchi ili kuhamasisha maendeleo ya sekta hiyo nchini. Maonesho hayo mwaka huu yatashirikisha washiriki 265 kati yao 33 ni kutoka nje ya nchi.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment