Arusha
Home » » TAARIFA YA KUKAMATWA KWA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BANGI MAGUNIA 50 NA WATUHUMIWA WANNE MKOANI ARUSHA

TAARIFA YA KUKAMATWA KWA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BANGI MAGUNIA 50 NA WATUHUMIWA WANNE MKOANI ARUSHA



Mkuu wa kitengo cha kuzuia na kudhibiti madawa ya kulevya Mkoa wa Arusha
Mrakibu wa Polisi Hamis Warioba akiwaonyesha waandishi wa habari
shehena ya mifuko 50 ya bangi iliyokuwa kwenye gari baada ya kukamatwa
tarehe 23/05/2012 wilayani Longido 
Mkuu wa kitengo cha kuzuia na kudhibiti madawa ya kulevya Mkoa wa Arusha
Mrakibu wa Polisi Hamis Warioba akihoji jambo kwa watuhumiwa hao.

(PICHA NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA)


MNAMO TAREHE 23/05/2012 MUDA WA SAA 9:00 ALASIRI
HUKO SINYA VILIMA SABA MPAKANI MWA KENYA NA TANZANIA KATIKA WILAYA YA
LONGIDO, ASKARI WA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI
WA WANYAMA PORI WALIFANIKIWA KUKAMATA WATU WANNE WAKIWA NA MIFUKO 50
YA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BANGI KWENYE GARI AINA YA CANTER DCM LENYE
NAMBA ZA USAJILI T.922 AFJ MALI YA ZEPHANIA S/O KAMBEI MKAZI WA NGARAMTONI.

MADAWA HAYO YALIKUWA YANASAFIRISHWA KUTOKA KATIKA
VIJIJI VILIVYOPO KANDO YA KANDO YA MLIMA MERU KUELEKEA NAIROBI NCHINI
KENYA KUPITIA NJIA ISIYO RASMI (MAARUFU KAMA NJIA YA PANYA) ILIYOPO
HUKO SINYA VILIMA SABA, NA BAADA YA KUONA HIVYO RAIA WEMA WALITOA TAARIFA
KWA ASKARI HAO NA HATIMAYE KUFANIKIWA KUWAKAMATA.

WATUHUMIWA WALIOKAMATWA KATIKA TUKIO HILO NI BABUU S/O LAIZER (34) MKULIMA,
MKAZI WA OLDONYOSAMBU,LOMNYAKI S/O LEKIBENGI
(30) MKULIMA , MKAZI WA OLDONYOSAMBU, JOHN S/O JOSHUA AMBAYE
NI UTINGO NA NI MKAZI WA OLDONYOSAMBU NA EDWARD S/O MOLLEL (27)
DEREVA NA NI MKAZI  WA OLDONYOSAMBU.

BADO JESHI LA POLISI MKOANI HAPA LINAENDELEA KUWAHOJI
WATUHUMIWA HAO ILI KUBAINI WAHUSIKA WENGINE NA PINDI UPELELEZI UTAKAPOKAMILIKA 
WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.

IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI
MKOA WA ARUSHA,

KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI

(SACP) THOBIAS ANDENGENYE

TAREHE 25/05/2012.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa