Arusha
Home » » MFANYABIASHARA WA MADINI KORTINI KWA KUMPIGA CHUPA MKEWE MBELE YA BABA MKWE

MFANYABIASHARA WA MADINI KORTINI KWA KUMPIGA CHUPA MKEWE MBELE YA BABA MKWE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na Woinde Shizza,Arusha


Mfanya biashara maarufu wa madini  jijini Arusha, Venance  Moshi
(30)amefikishwa Mahakamani na kusomewa maelezo ya awali katika kesi
 inayomkabili ya kushambulia na kumjeruhi  mkewe kwa chupa usoni ,wakiwa
wanasuluhishwa na baba mkwe, mgogoro wa ndoa yao.



Mbele ya hakimu , Devota Msofe wa mahakama ya wilaya .Arusha ,mwendesha
mashtaka wa serikali ,Agnesi Hyera alieleza mahakama hiyo kuwa mnamo marchi
11 mwaka 2016 katika maeneo ya Moshono kwenye usuluhishi wa mgogoro wa ndoa
yao ,mshtakiwa alinyanyua glasi na kumpiga kwenye jicho la kulia
mlalamikaji (mkewe) Agnesi Joseph (30)iliomjeruhi vibaya  .


Mwendesha mashitaka aliieleza mahakama hiyo kuwa kuwa hatua hiyo
ilimsabishia mlalamikaji atokwe na damu nyingi na baadae kutoa taarifa
kituo cha polisi ambapo mtuhumiwa alitiwa mbaroni na baadae kufikishwa
mahakamani.



Baada ya kusomewe maelezo hayo mshitakiwa  huyo alikana mashtaka ,na hakimu
Msofe  alipanga siku ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo,baada ya upande
wa jamhuri kudai kuwa wapotayari kwa usikilizwaji wa kesi hiyo.



Katika shauri hilo la jinai namba 438 la mwaka 2016 ,upande wa jamhuri
unatarajia  kuwasilisha mashahidi watatu na vielelezo kadhaa ikiwemo hati
ya polisi(PF3) , hati ya daktari pamoja na picha za jeraha .Kesi hiyo
imepangwa kusikilizwa february  6 ,mwaka huu ,saa tatu asubuhi.



Aidha katika hatua nyingine ,shahidi namba moja wa kesi hiyo ,Agnes Joseph
anatarajia kufungua kesi nyingine ya kudai talaka kwa mumewe huyo
waliyefunga naye ndoa mwaka 2012 baada ya ndoa yao kukumbwa na migogoro ya
mara kwa mara huku akiambulia kipigo na vitisho.



Alisema  ameishi na mumewe huyo katika mazingira ya migogoro na wamekuwa
wakisuluhishwa mara kadhaa bila mafanikio,

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa