Home » » Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo:“Ni kweli mimi ni muumini wa Lowassa,ila pale (mkutanoni) sikumtaja kwa sababu najua chama kina taratibu zake na muda wa mchakato wa kumpata Rais haujafika.”

Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo:“Ni kweli mimi ni muumini wa Lowassa,ila pale (mkutanoni) sikumtaja kwa sababu najua chama kina taratibu zake na muda wa mchakato wa kumpata Rais haujafika.”
MBUNGE wa Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo 
----
MBUNGE wa Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo ametangaza kuchukua
kile alichokiita uamuzi mgumu ili kuhakikisha kuwa Mbunge wa Monduli
(CCM), Edward Lowassa anamrithi Rais Jakaya Kikwete katika Uchaguzi Mkuu
wa mwaka 2015.
Shelukindo alitoa kauli hiyo Jumapili wakati
akiwasalimia wakazi wa Monduli baada ya kukaribishwa kuchangia ujenzi wa
Hosteli ya KKKT katika sherehe za kukaribisha Mwaka Mpya zilizofanyika
nyumbani kwa Lowassa ambazo pia zilihudhuriwa na makada kadhaa wa CCM.
Jana alipoulizwa kuhusu kauli hiyo, Shelukindo
alisema:“Ni kweli mimi ni muumini wa Lowassa, ila pale (mkutanoni)
sikumtaja kwa sababu najua chama kina taratibu zake na muda wa mchakato
wa kumpata Rais haujafika.”
“Niliposimama niliwaeleza kuwa nisingeweza
kuchangia fedha nyingi kwa sababu watu wangu wana njaa huko Kilindi. Pia
kule (Kilindi) tunaendesha harambee ya aina hiyohiyo. Ila nikawaambia
zawadi yangu kwa Wanamonduli ni kufanya uamuzi mgumu ili mwaka 2015
apatikane Rais mzalendo na anayeweza kufanya uamuzi mgumu na kwa
wakati.”Kwa habari zaidi Bofya na Endelea........>>>

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa