Arusha
Home » » POLISI YAMSAKA MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI

POLISI YAMSAKA MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI



Na Gladness Mushi wa Fullshangwe-Arusha

JESHI  la Polisi
limempa masaa machache Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Bw Joshua Nassari
na endapo kama hatajisalimisha kwa jeshi hilo basi nguvu  zaidi zitatumika katika kumsaka kwa kuwa
Mbunge huyo ametoa lugha za uchochezi kwa wananchi juzi katika mkutano ambao
ulihudhuriwa na viongozi wa juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)



Hayo yalisemwa na Naibu Kamishna wa jeshi la Polisi hapa
nchini Bw Isaya Mngulu wakati akiongea na vyombo vya habari mapema jana jijini
hapa

Kamanda Mngulu alisema kuwa Mbunge huyo alitoa matamko hayo
katika viwanja vya NMC  juzi ambapo
alidai kuwa Rais hapaswi kufika katika kanda ya kaskazini hasa katika
jimbo hilo endapo kama atashindwa kufuatilia sakata la mauaji  ya aliyekuwa kada wa  Chadema kwa haraka sana

Aidha aliongeza kuwa
mbali na mbunge huyo kusema maneno hayo pia aliwaambia wananchi

waliokuwa umati mkubwa sana
katika maeneo ya viwanja vya NMC kuwa
yeye ndiye atakayekuwa Rais
wakati  Waziri mkuu atakuwa ni

Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Bw Goodbless Lema hali ambayo inaonesha kauli
za uchochezi

“Hizi kauli ni za uchochezi mkubwa sana na tumejaribu
kumtafuta kwa kila njia lakini hajaonekana na sasa tunatumia vyombo vya habari
kumtafuta na endapo kama hatajitokeza tutatumia mbinu za kijeshi kumsaka ili
ajibu alichokikiri”alisema Bw Mngulu

Akiongelea sakata la baadhi ya wanachama wa Chadema kudai
kuwa wanatishiwa kuwawa na watu wasiojulikana kuwa madai hayo ni ya uongo na
wanaotuma na kusambaza ujumbe mfupi(SMS) ni
makada wa Chadema na mpaka sasa Jeshi hilo limeshawabini

“ninachotaka kuwaambia ni kuwa hawa watu wa Chadema
wanatakiwa kujua sisin Polisi sio watoto wadogo wa kudanganywa tulichokijua ni
kuwa wanatumiana SMS wao wenyewe  na
tunafanya upelelezi na tutahakikisha kuwa tunawatia Mbaroni”alisema Bw Mngulu

Awali alisema kuwa mpaka sasa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha
limefanikiwa sana
kuwatia Mbaroni watu12 ambao walihusika na Mauaji mbalimbali katika eneo la
Meru ambapo watu 3 wameshafikishwa mahakamani huku wengine wakiwa wanaendelea
na uchunguzi  katika  tukio la kuuwa vibaya kwa Kada wa Chadema
wiki chache zilizopita.

Pia alisema kuwa mbali na kuweza kuwashikilia watu 12 ambao
wanahusika na  mauaji ya Kada wa Chadema
pia bado jeshi hilo linaendelea na upelelezoi zaidi ili kuweza kuwatia mbaroni
pia waliohusika na mauaji ya bibi kizee Bi Martha Joseph(77) kwa madai kuwa
alikuwa ni mchawi katika eneo la Nkoaranga


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa