Home » » SERIKALI: TANZANIA KUWEKEZA ZAIDI KATIKA TAFITI ZA MAGONJWA MBALIMBALI

SERIKALI: TANZANIA KUWEKEZA ZAIDI KATIKA TAFITI ZA MAGONJWA MBALIMBALI



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa 26 wa
mwaka wa Wadau wa Sayansi  ulioandaliwa
na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadam (NIMR), ulioanza jana
Aprili 16, 2012 jijini Arusha. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.
Na  Gladness Mushi wa Fullshangwe-ARUSHA

SEREKALI imesema kuwa kwa sasa inawekeza zaidi katika
masuala ya tafiti  za magonjwa mbalimbali
jambo ambalo litaweza kupunguza na kuhudumia vema jamii mbalimbali za
watanzania

Hayo yamebainishwa jijini hapa na Makamu wa Raisi wa
jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Gharib Bilal wakati akifngua mkutano
kongamano la 26 kwa wadauj wa taasisi  ya
utafiti wa magonjwa ya binadamu(NIMR) mapema jana

Dkt Bilali alisema kuwa kwa mfumo huo wa Serikali kuweza
kuwekeza zaidi katika tafiti za magonjwa ya binadamu kutasaidia kwa kiwango
kikubwa sana hata kupata vyanoz halisivya magojwa ambayo yanasumbua Jamii

Aliongeza kuwa mbali na kufanikiwa kuwekeza zaidi katika
masuala ya tafiti ambayo yanafnywa na baadhi ya watafiti hapa nchii lakini pia
Serikali nayo imejipanga kuhakikisha kuwa inaendelea kuwa na wataalamu wengi
zaidi ambao nao kwa kiwago kikubwa sana wataweza kusadia jamii

“kwa sasa tumejipanga kuhakikisha kuwa kila mahala tunakuwa
na watafiti ambao wataweza kufanya chunguzi mbalimbali na kasha kubaini vyanzo
hali ambayo itatufanya tuweze kufikia malengo yetu ya kupambana na aina
mbalimbali za magonjwa ambayo tumekusudia

Pia aliongeza kuwa kwa sasa Serikali nayo imefanikiwa kukabiliana
na changamoto mbalimbali ambazo zimo kwenye jamii kama vile vifo vya mama na mtoto,
pamoja na gonjwa ambalo lilikuwa linasumbua sana ,Malaria

Alifafanua kuwa kwa sasa ndani ya changamoto hiyo magonjwa
ya Malaria yamepungua kwa kiwango cha hali ya juu sana pamoja na vifo vya mama
na mtoto jambo ambalo ni faraja kwa Serikali kutokana na malengo yake ambayo
yamekusudiwa

Awali mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo ya  taifa ya utafiti wa magonjw yabinadamu , Dkt
Mwele Malecela  alisema kuwa kwa sasa
ndani ya nchi ya Tanzania kuna umuhimu mkubwa sana wa watalaamu kuweza kufanya
tafiti  ambazo zitakuwa pamoja na Takwimu
hali ambayo itachangia kwa kiwango kikubwa sana
watalamuj hao kuweza kufanya kazi kwa uraisi sana.


Dkt Mwele alisema kupitia Tafiti na Takwimu za magonjwa
mbalimbali wataweza kujua na kubaini kasi ya magonjwa hata yanayoambukiza kwa
kasi sana jambo ambalo nalo litaweza kupatiwa ufafanuzi kwa ikwiango cha juu
sana.


0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa