Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akipokelewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TPRI) Dkt Margaret Mollel wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Katikati) akisikiliza
maelezo ya namna ya ufanyaji kazi mara baada ya kutembelea Kitengo cha
Unyunyuziaji wa Viuatilifu alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TPRI) Dkt Margaret Mollel.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Kushoto) akitembelea baadhi ya maeneo ya Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akitumia mashine ya Kunyunyizia viuatilifu wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza kwa makini
maelezo ya namna maabara ya kupima masalia ya Viuatilifu inavyofanya
kazi wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017.
Na Mathias Canal, Arusha
Watumishi
wa serikali wanaofanya kazi katika Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya
kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides
Research Institute-TPRI) wametakiwa kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa
Weledi, Bidii na Nidhamu.
Kauli
hiyo imetolewa Leo 16 Disemba 2017 na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo
Mhe Mary Mwanjelwa alipokuwa akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo wa
Taasisi hiyo wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha.
Mhe
Mwanjelwa aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii, Juhudi,
Maarifa na Ubunifu kwani kufanya hivyo kutathibitisha matokeo chanya
katika utendaji wao huku akiwapongeza kwa kufanya kazi kwa moyo na
uvumilivu mkubwa pamoja na kuwepo kwa kadhia ya upungufu wa watumishi.
Sambamba
na Taasisi hiyo kuwa na jukumu la kufanya utafiti, kutoa huduma za
usajili na udhibiti wa viuatilifu, Mafunzo kuhusu visumbufu na kufanya
hifadhi ya Bioanwai husika ili kuchangia uhakika wa chakula lakini pia
ina jukumu la kuendelea na kudumisha mashamba darasa kwa ajili ya
Utafiti na mafunzo kwa wadau hususani katika matumizi sahihi na salama
ya Viuatilifu.
Aidha,
Alimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TPRI) Dkt Margaret Mollel kwa
kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kusimamia Taasisi hiyo ikiwa ni
pamoja na umakini wa Taasisi katika kufanya kazi zake katika kipindi cha
miaka 10 ya utekelezaji wa muundo mkakati wa TPRI (2005-2015).
0 comments:
Post a Comment