Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo akitoa hotuba fupi katika hafla fupi ya uzinduzi wa mafunzo ya shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo mapema jana.
Meja jenerali Paul Peter Masao ambaye ni mkuu wa chuo cha mafunzo ya maafisa wanafunzi jeshi la ulinzi la Tanzania(TMA) akizungumza kwenye hafla hiyo jana.
Katibu mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa Florens Turuka akizungumza katika uzinduzi wa uzinduzi wa shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo
Kaimu mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha, Dokta Faraji Kasidi akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alisema mahusiano kati yao na chuo hicho cha kijeshi yameanza muda mrefu ambapo wao wamekuwa wakifundisha askari hao mafunzo ya kiraia.
kushoto aliyevalia suti ni Profesa Johannes Monyoambaye aliwahi kuwa mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha(IAA)
Wanafunzi wa mafunzo ya shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo mapema jana.
Picha ya pamoja.
Na Pamela Mollel,Monduli
Katibu
Mkuu wa wizara ya ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dkt Florens Turuka
amesema kuwa jeshi hilo hivi sasa limejipanga katika kukabiliana na
changamoto za ulinzi na usalama kwa kuwapatia askari wake mafunzo maalumu ya sayansi ya kijeshi.
Aliyasema
hayo Jana wakati akizungumza katika uzinduzi wa shahada ya kwanza ya
sayansi ya kijeshi inayotekelezwa na chuo cha uhasibu Arusha kwa
kushirikiana na Chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli (TMA).
Alisema
kuwa, kumekuwepo na matishio mengi ambayo yamekuwa yakijitokeza Kwa
namna tofauti ambapo hivi sasa matishio hayo yamegeuka na kuhamia kwenye
mitandao, hivyo kama jeshi wana wajibu wa kujipanga zaidi kwa kuwaandaa maaskari ili waweze kukabiliana na hali hiyo mahali popote.
Dkt
Turuka alisema kuwa, wao Kama jeshi ni wajibu wao kujipanga mapema kwa
kuangalia namna ya kuwajengea uwezo hasa katika maswala ya sayansi na
teknolojia ili kuboresha ulinzi na usalama hapa nchini.
Kwa
upande wa Mkuu wa majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo alisema kuwa
wamekuwa wakitoa mafunzo hayo kwa maaskari wake kulingana na mabadiliko
ya kidunia hasa katika maswala ya
sayansi na teknolojia kwani ni eneo ambalo linahitaji elimu kubwa
zaidi. Alisema kuwa, ni lazima wasonge mbele na kwenda na wakati kwani
wasipofanya hivyo watabaki nyuma na kamwe hawataweza kukabiliana na
vitisho vilivyopo hivi sasa.
Naye
Mkuu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli (TMA), Dokta Paul Massao
alisema kuwa, wamekuwa wakitoa masomo ya kijeshi na kiraia ili kuwaandaa
vijana katika hatua ya ngazi za juu zaidi kielimu ambapo kwa kuanzia kozi hiyo watahiniwa 158 wataanza kozi hiyo mapema.
Kwa
upande wa Kaimu mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha, Dokta Faraji Kasidi
alisema kuwa, mahusiano kati yao na chuo hicho cha kijeshi yameanza muda
mrefu ambapo wao wamekuwa wakifundisha askari hao mafunzo ya kiraia ambayo yamekuwa yakileta manufaa makubwa Sana.
0 comments:
Post a Comment