Home » » WAUZA NYAMA WATENGA FEDHA KWA AJILI YA KUSAIDIA KULIPIA KAYA MASKINI BIMA YA AFYA

WAUZA NYAMA WATENGA FEDHA KWA AJILI YA KUSAIDIA KULIPIA KAYA MASKINI BIMA YA AFYA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
Na Woinde Shizza,Arusha

Umoja wa wauza nyama jijini Arusha (wanjamuco) umetenga shilingi laki tano kwa ajili ya kulipia bima ya afya katika kaya mbili kwa kila kata zinazoishi katika mazingira magumu ili kuwawezesha kupata matibabu bure katika zahanai na hospitali zote za jijini humo. 

Mwenyekiti wa umoja huo Alex Lasiki, amesema hayo leo jijini Arusha wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja wa umoja huo.

amesema katika kusherehekea mwaka mmoja wa umoja wao, wanachama wamekubaliana kuwa watenge kiasi hicho kutoka kwenye mapato yao waliyoyapata kwa mwaka mzima ili wawezeshe familia mbili zenye watu 12 zinazoishi katika mazingira magumu kupata bima ya afya ijulikanayo kama lita inoyosimamiwa na jiji la Arusha .
Lasiki ameongeza, kupitia bima hiyo familia hizo zitapata huduma za matibabu bure, kwenye zahanati au hospitali yoyote ambapo fedha hizo ni sehemu ya kurudisha faida wanayoipata katika jamii wanayoiudumia kupitia biashara yao ya kuuza nyama.

Pamoja na mchangohuo, Lasiki amesema, moja wa huo pia unakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ya uanzishwaji wa mabucha feki haswa eneo la Samunge yasiyokuwa na viwango yanayouza nyama ambazo hazina viwango hivyo kuhatarisha afya za walaji.

Mbali na hilo, Wanjamuco wanaiomba serikali iwajangee kiwanda cha kuchakata ngozi kwani kwa sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya sehemu màalum ya kuuzia ngozi kutokana na serikali kupiga marufuku usafirishwaji wa ngozi hizo nje ya nchi.

Naye Diwan wa Kata ya Olerian, Zakaria Absalum, akizungumza katika maadhimisho hayo amesema, kero kubwa ambazo zinawakabili wafanyabiashara wa nyama jijini hapo ni pamoja na usafirishwaji wa ng'ombe kwenda nchi jirani ya Kenya ambapo, wanaosafirsha hawalipi kodi na wanakifika mpakani mtu mmoja mwenye leseni yeye ndio analazimika kuingiza mifugo yote kwenda kufanya biashara kwenye ardhi ya kenya bila kuilipia ushuru na hivyo kuisababishia serikali hasara.

Absalum ambaye pia ni mfanyabiashara wa nyama ameongza kuwa, kutokana na kero hiyo ni vema serikali ikajenga mnada maalum eneo la Namanga ili ilete ushindani kwa wafanyabiashra hao kuziba mianya ya wale wanaoingiza mifugo bila kuwa na leseni za biashara.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa