Home » » MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI SITA YENYE THAMANI YA SH. 1.2 BILIONI WILAYANI MONDULI

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI SITA YENYE THAMANI YA SH. 1.2 BILIONI WILAYANI MONDULI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa,Salome Mwakitalima akivalishwa Skafu na mmoja wa watoto wa chipukizi wakati wakiingia wilaya ya Monduli kutoka wilaya ya Arusha. 
Mkuu wa wilaya ya Monduli,Idd Kimanta(kulia)akimpokea mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa. 
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru,Amour Hamad Amour akitoa ujumbe wa Mwenge baada ya kufungua nyumba ya watumishi wa Afya katika Kijiji cha Mswakini Juu wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha kwa gharama ya Sh 53 milioni. 
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru,Amour Hamad Amour akimkabidhi mmoja wa wananchi Chandarua kwaajili ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa Malaria wakati kufungua nyumba ya watumishi wa Afya katika Kijiji cha Mswakini Juu wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha iliyojengwa kwa gharama ya Sh 53 milioni,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Monduli,Idd Kimanta. 
Wananchi wa kijiji cha Mswakini Juu wakishangilia ujumbe wa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 


Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa,Amour Hamad Amour amezindua miradi sita ya maendeleo yenye thamani ya Sh.1.2 Bilioni.

Miradi hiyo ni wa maji katika Kijiji cha Meserani Juu ambao usanifu wake ulianza mwaka 2013 na umekamilika kwa gharama ya Sh 513 milioni wakati serikali imechangia Sh 444.5 milioni ,halmashauri ya Monduli imechangia Sh 66.6 milioni na wananchi Sh 2.2 milioni.

Pia kiongozi huyo amezindua mradi wa barabara yenye urefu wa kilometa 11kutoka Monduli hadi Kijiji cha Lendikinya uliofadhiliwa na Mfuko wa Barabara(Road Fund) kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kwa jumla ya Sh 272.6 milioni.Imeelezwa kukamilika kwa wa mradi huo kutarahisisha usafiri na kutachochea shughuli za wananchi kujiletea maendeleo na kusadifu azma ya serikali ya kuwa na uchumi wa kati wa Tanzania ya viwanda.

Pia kiongozi huyo amefungua nyumba ya wafanyakazi wa afya katika Kijiji cha Mswakini Juu iliyojengwa kwa ushirikiano wa nguvu za wananchi na halmashauri ya wilaya ya Monduli kwa gharama ya sh 53 milioni.

Miradi mingine iliyozinduliwa ni kiwanda kidogo cha kuchakata chakula cha mifugo katika Kijiji cha Mungure na uzinduzi wa mradi wa MMES II (SEDP II)katika shule ya Sekondari Oltinga kwa gharama ya Sh 225 milioni
Imeandaliwa na mtandao wa www.rweyemamuinfo.blogspot.com

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa