wamama wa kijiji cha Sambaru wakiendelea kutwanga mawe kwa ajili ya kuweka tayari kwa kupatikana madini ya ya zahabu
baadhi ya vijana wa kijiji cha sambaru
Na Woinde Shizza,Singida
Zaidi ya vijana 60 wa kijiji cha
Sambaru kata ya Ikungi wilayani Igungi
mkoani Singinda wamemlalamikia mwekezaji wa kampuni ya Sambaru
Gold Mining kwa kitendo cha kuwarusha fedha za malipo ya kazi walikuwa wakimfanyia mgodini kwake
Wakiongea na waandishi wa habari kijijini hapo
baadhi ya vijana hao walisema kuwa wamefanya kazi katika kampuni hiyo kwa
kipindi cha mda mrefu lakini muwekezaji huyo ajawalipa ela zao na badala yake amewafukuza kazini hapo bila
kuwalipa malipo yoyote .
Mmoja wa vijana hao aliyejitambulisha
kwa jina la Saidi Hassan alisema kuwa walishapeleka malalamiko yao kwa viongozi
wa kijiji lakini hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa hivyo wameiomba serikali
iwasaidie ili wapate mafao yao kwani fedha hizo walikuwa wanazitegemea katika
kuwasaidia katika majukumu mbalimbali ya kifamilia.
“tumekuwa tunamfata muwekezaji huyu
na kumuomba atulipe fedha zetu lakini
amekuwa anatukana na kusema atudai ,mbaya zaidi kunawakati alifikia hatua ya
kukamata baadhi ya wenzetu ambao wanamdai na kuwapeleka polisi,”alisema Saidi
Kwa upande wake kijana mungine
aliyejitambulisha kwa jina la Fredy John alisema kuwa kunakipindi walishawahi
kumpeleka polisi alipofika na kuulizwa kama vijana hao wanamdai alikuabali na
akahaidi kuwalipa na aliomba mda na akapewa kimaandishi lakini ,muda huo
umepita na hadi leo vijana hao awajalipwa na amefikia hatua ya kuwakana kabisa
Gazeti hili lilimtafuta mwenyekiti wa
kijiji hicho cha Sambaru Mfaume Hassan ili kubainisha kama anataarifa za vijana hawa
nae alisema kuwa ni kweli anataarifa za vijana hawa na alishamtumia mmiliki wa
kampuni hiyo taarifa za kuwalipa vijana hawa lakini hajateleza hivyo ameamua kupeleka swala hili katika
ngazi za juu ili wamsaidie
“sisi kama kijiji tumekuwa tuna
utaratibu wa kuwapa vijana wawekezaji
hawa nah ii inatokana na uhitaji wa muwekezaji ,unakuta muwekezaji anataka
vijana wa kumsaidia kazi uko mgodini kwake analeta barua katika ofisi ya
kijiji na sisi tunampa vijana na ndio utaratibu uliofanywa sasa
muwekezaji huyu kaja kuchukuwa vijana lakini cha kushangaza wamefanya kazi
mgodini kwake lakini ajawalipa mpaka leo na mbaya zaidi akifatwa anasema kuwa
adaiwi kitu ambacho sio cha kweli mimi kama kiongozi wa kijiji nikishirikiana
na wenzangu tutajitaidi kufuata sheria ili vijana hawa walipwe ela zao na hadi
sasa navyoongea nilishampa taarifa mkuu wa wilaya”alisem Mwenyekiti wa kijiji
Mfaume Hassan
Gazeti hili lilimtafuta mmiliki wa kampuni ya Sambaru Gold Mining Ahamed Magoma kujibu
tuhuma hizi nae alisema kuwa yeye kama yeye adaiwi na kijana yeyote Yule
wa kijiji cha Sambaru ,na kama kuna mtu anae mdai afuate vyombo husika vya sheria akamdai
“mimi sidaiwi na kijana yeyote Yule vijana
wangu wote ambao nawaajiri nawalipa
vizuri na wengine wapo kazini hadi sasa,pia mimi sijawai kwenda kijijini
kutafuta kijana wa kunifanyia kazi na napenda kusema ivi kama kuna mtu ambae
ananidai afuate sheria ,aje na vielelezo
anidai na kama ni kweli nitamlipa ila
sidaiwi na mtu yeyote “alisema Magoma
Akiongelea swala hilo mkuu wa wilaya
ya Ikungi Miraji Mtaturu alisema kuwa swala hilo
alishalipokea kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji cha Sambaru na alimuagiza aandike idadi ya vijana hao
pamoja na majina yao ili ayafanyie kazi ,aidha pia alisema kuwa atamuandikia
barua ya kumuita ofisini kwake mmiliki wa mgodi huo wa Sambaru Gold Mining .
0 comments:
Post a Comment