Na Woinde Shizza,Arusha
Wagombea wa nafasi mbalimbali za ungozi ndani ya chama cha
mapinduzi wilaya wa Arusha wametakiwa kufuata kanuni na sheria za
zilizowekwa na chama hicho.
Hayo yamebainishwa na katibu wa chama cha mapinduzi wilaya
ya Arusha Dr, Ramathani Dallo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini
kwake kuhusiana na tuhuma za kuwepo na
baadhi ya wagombea kuja kwenye usahili na watu wanaodaiwa sio wagombea bali ni
waganga wa kienyeji
Alisema kuwa ni muhimu sana wagombea wakifuata kanuni
taratibu na sheria zilizowekwa katika
uchaguzi kwa mujibu wa kanuni ya muongozo wa uchaguzi ya mwaka 2010
Alisema kuwa yeye binafsi ajawaoana watu hao wanaodaiwa ni
waganga wa kienyeji na usahili ulienda
vizuri na k atika kipindi hichi uchaguzi
unaendelea vyema ,huku akibainisha kuwa iwapo kutakuwa na mgombea yeyote ambae
atakwenda kinyume na sheria ya uchaguzi atamuaonea huruma bali atuakali zidi
yake itachukuliwa .
“nasema kwakweli ili swala na mgombea wa UWT kuja na mganga wa kienyeji kwenye
usaili sijaliona ila ukweli napenda kuchukua nafasi hiii kuwasihi iwapo
tutamkamata mgombea yeyote Yule anaekwenda kinyume na sheria tutamchukulia
hatua kali za kisheria ikiwemo kuinta kikao kama jambo ni gumu sana pia
itatulazimu tumkate jina lake na asiwepo kwenye kinyanganyiro chochote”alisema
Dr,Dallo
Alizitaja baadhi yakanuni kuwa ni pamoja na kutofanya kampeni ,kukusanya watu kufanya mikutano isioyo rasmi kichama pamoja na nyingi
Aidha akiongelea baadhi za uchaguzi zilizopita alisema kwa
upande wa uchaguzi wa kata ,mitaaa umemalizika vizuri sasa ivi ndio wanaendelea
na maeneo mengine yaliyobaki
Awali baadhi ya wagombea ambao hawakutaka majina yao
yaandikwe walisema kuwa kuna mmoja wa mgombea mwenza sik u ya usahili alikuja
akiwa na mganga wa kienyeji kitu ambacho ni kinyume na sheria ya uchaguzi
0 comments:
Post a Comment